Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasanii, Madansa lini wataacha kukopi vya watu?

Konde X Mondi Wasanii, Madansa lini wataacha kukopi vya watu?

Wed, 22 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muziki wa Bongo fleva na sanaa kwa ujumla imekuwa ikizidi kufanya vizuri kila kukicha katika nyanja tofauti tofauti.

Wasanii wamekuwa wakitoa kazi ambazo zimekuwa zikifanya vizuri kwenye 'platform' mbalimbali pamoja na chati za muziki ndani na nje ya nchi.

Ubunifu ni kitu ambacho kimekuwa kikifanya kazi ya sanaa kuvutia na kupendwa na mashabiki.

Ubunifu na upekee katika kila kazi ya sanaa hasa muziki pamoja na Madansa kwa kiasi chake umepungua kutokana na kukopi kwa asilimia kubwa kutoka sehemu nyingine.

Wasanii wakielemea zaidi kwenye 'trending' za muda kuliko ubunifu utakaodumu kwa kipindi kirefu na kuendelea kufanya vizuri zaidi kwa kazi zao.

Muziki wa amapiano ambao asili yake ni Afrika ya Kusini umeendelea kushika kasi katika bongo fleva yetu kuanzia ku 'sample' biti mpaka aina ya uchezaji.

Kwasasa sio waimbaji tena hata madansa wamehamia Afrika kusini kukopi mpaka aina za kucheza hata kwenye ngoma za Bongo Fleva.

Dansa asipocheza staili ya 'Umlando' 'Zekethe' Gwaragwara, Vosho, dakiwe, Sika Lekhekhe, n.k basi ataonekana hajui kucheza.

Lini Muziki wa Bongo fleva utatumika na watu wengine wa 'sample' vitu vyetu kama sisi tunavyochukua kutoka kwao?

Ni wakati gani madansa wa hapa nchini watagundua style mpya na nzuri za kucheza ambazo zitafanya vizuri hapa nchini na Kimataifa? ili waache ku 'copy na kupaste'?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live