Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasanii Cheko Kama Lote na Rais Samia

Samia Wasanii Rais Samia Suluhu

Thu, 27 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

LEO ni maazimisho ya siku ya kuzaliwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan; “Happy Birthday Mama” ndiyo habari ya mjini.

Pamoja na watu wengi makumi kwa mamia kama siyo maalfu na mamilioni kumtakia heri Rais Samia katika siku yake ya kuzaliwa wasanii na mastaa mbalimbali nao hawakubaki nyuma.

Kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii wengi wameungana na Rais Samia kushangweka pamoja naye katika tarehe hii ambayo imemfikishia rasmi umri wa miaka 62.

Hata hivyo, jicho letu mitandaoni limepitia baadhi ya kurasa za mastaa, wasanii na kukuta hawajaandika chochote cha kumtakia heri rais Samia.

Yote maisha ila upendo kwa mama udumu miyoni mwa Watanzania wote na Kazi Iendeleee.

Msanii Juma Jux kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika: “Happy Birthday Mama Yetu @samia_suluhu_hassan, Mungu Akupe Maisha Marefu na Afya Bora, Tuendelee Kujenga nchi yetu, Tunakupenda.

Msanii Zuchu kamtakia heri rais Samia kwa kuandika: “Happy birthday to my president@samia_suluhu_hassan May Allah give and increase your strength Mama, Amin.

Diamond: “Happy Birthday Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. @samia_suluhu_hassan ….Asante kwa kufanya Tanzania inafuraha sasa…Mwenyezi Mungu Akupe Umri mrefu zaidi ili Watanzania tuzidi kufaidika na Neema za uongozi wako Bora.

Basi hawa ni kwa uchache lakini wako wasanii wengi, unaweza kupitia kwenye kurasa zingine na kuona walichoandika mastaa na watu maarufu kuhusu siku ya kuzaliwa ya Rais Samia.

Usipoona wowote basi ujue ndiyo wale niliosema bado wanafikiria wamuwishi au waache tu maisha yaendelee.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live