Msanii wa Hip Hop, Ibrahim Mussa 'Roma' amesema wasanii wa Bongo wanapendana tofauti na watu wengi wanavyoamini mtaani.
Roma ametoa ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa X na kueleza uzoefu alioupata akiwa pande za Marekani.
"Nikikaa na watu Wa Mataifa mengine Wananambia Industry Yenu Ya Music Bongo Wasanii Wanapendana sana, Imagine Nawaona Wasanii zaidi ya 20 wanapanda Bus Moja/Ndege moja wanasafiri pamoja City To City kwa Masaa 6-7 Bila Vita Wala Kugombana, kwetu huwezi kuona kitu kama hiko! Mimi ninachomekea nawaambia na unakuta Mbuzi anakaa siti moja na Chui na wakifika wanalala hotel moja Woote.
"Nways ukitafakari kwa undani utaona jamaa ana-make sense sana! Lakini sisi Maskani tunaamini na tunakiri kuwa wasanii wetu hawapendani!!"