Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasanii 200 waelekea Arusha kuwania tuzo za Serikali

WhatsApp Image 2022 12 14 At 20.jpeg Wasanii 200 waelekea Arusha kuwania tuzo za Serikali

Thu, 15 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wasanii wa filamu Mkoa wa Dar es salaam wapatao 200 wameanza safari leo Desemba 14,2022 kuelekea jijini Arusha kushiriki Usiku wa Tuzo za Filamu zilizoandaliwa na Serikali kushirikianana Bodi ya Filamu.

Akizungumza leo na Michuzi Blog, Msanii wa filamu nchini Shamira Ndwangila a.k.a Bi.Star amesema kwa upande wake ana matumaini ya kurejea Jijini Dar es salaam akiwa na tuzo huku akiwaomba mashabiki zake kuendelea kumpigia kura kwa siku zilizobakia kuelekea fainali hiyo.

"Nimepata fursa ya kuonekana mchango wangu kwa takribani miaka 24 hatimae kazi zangu ambazo nimezifanya nikiwa na uhusika tofauti kuingia kwenye tuzo,hivyo nawapongeza Serikali kwa kuweka tuzo,"amesema Bi.Stara.

Msanii huyo wa filamu ameingia kwenye vipengele vya Msanii bora wakike pamoja na Msanii bora wa kike chaguo la watazamaji kupitia kazi ya "Kombolela" ambayo amevaa uhusika wa Mwanadawa.

Bi.star ameeleza safari ya kuelekea jijini Arusha inakwenda kuongeza chachu na ufanisi katika kazi za sanaa na tasnia nzima kwa ujumla kwani kuna kongamano linatarajiwa kufanyika Ngurudoto kwa lengo la kuwapa elimu na fursa wasanii wote wakiwemo washiriki wa tuzo hizo katika kutengeneza kazi zenye ubora kufikia soko la Kimataifa ikiwemo Netflix.

Pia ametolea ufafanuzi wa tuhuma za mtayarishaji wa tamthilia ya Kombolela, Salum Majagi kuwajia juu waratibu wa tuzo hizo kwa kutokuwepo kwa jina lake katika kipengele cha Mtayarishaji bora wakati wasanii wake aliowaongoza wamefanikiwa kuwepo kwenye vinyang'ayiro Sita kwenye tuzo hizo.

Wasanii kutoka Tamthilia ya Kombolela ambao wameimgia kwenye kinyang'anyiro cha kuwania tuzo hizo msanii bora wa kike ni Mwadawa, Msanii bora wa kike chaguo la watazamaji Mwadawa (Kombolela), Msanii bora wakiume chaguo la watazamaji Mzee Kikala, Msanii bora wa kiume Kobisi kikala.

Aidha tamthilia bora (Kombolela) pamoja na msanii Mpambe wa kiume Kobisi Kikala kutokea tamthilia ya (Kombolela), wimbo bora wa tamthilia (Kombolela) muimbaji akiwa Songoro.

Baadhi ya wasanii hao waliosafiri leo kwenda Arusha ni Kobisi Kikala, Single Mtambalike maarufu kama Rich Rich ,Dino, Mtitu,Brenda,Muhogo Mchungu,seif Mbembe,Nikita pamoja na Swebe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live