Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasafi yaleta balaa! Yanga yaufuta mchezo, Bodi yazuia

90031 Wasafi+pic Wasafi yaleta balaa! Yanga yaufuta mchezo, Bodi yazuia

Fri, 27 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

UAMUZI wa Uwanja mpya wa kuchezea mechi kati Yanga na Tanzania Prisons umezua utata baada ya Yanga kutoa tamko kwamba mchezo huo umefutwa huku Bodi ya Ligi (TPLB) ikisema hapana na mchezo upo palepale. Afisa Mhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kutokana na hali ya Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya ulivyoharibiwa na tamasha lka muziki lililofanyika usiku wa kuamkia leo wamekubaliana pande mbili kutocheza mchezo huo. Katika taarifa yake Nugaz amesema kikao cha makubaliano hayo ni kati yao na Prisons sambamba na maafisa wa usalama wa mchezo huo na kwamba wakati wowote timu yao itarejea jijini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo dhidi ya Biashara United. Hata hivyo wakati Nugaz akitoa msimamo huo Bodi ya Ligi imesema mchezo huo haujafutwa na kwamba wanatafuta uwanja mwingine utakaotumika badala ya Sokoine. Afisa Mtendaji Mkuu wa TPLB, Boniface Wambura amesema bado wapo katika mchakato wa kutafuta uwanjha mbadala na kwamba mechi hiyo lazima ichezwe kesho hiyohiyo. Mkanganyiko huo umetokana na Uwanja wa Sokoine kuharibiwa vibaya sehemu ya kuchezea kutokana na watu waliohudhuria tamasha la muziki lililofanywa na mwanamuziki Rayvany.

Chanzo: mwananchi.co.tz