Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasafi wamemvunjia heshima Juma Nature - 20-Percent

Nature Percent Juma Nature na 20-Percent.

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Akizungumza na moja ya chombo cha habari cha kuaminika hapa nchini, mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva nchini, 20-Percent amesema amesikitishwa na kitendo cha Wasafi kumtaka msanii mwenzake Juma Nature akafanye shoo kwenye Tamasha lao kwa kiasi cha laki tano.

20-Percent amesema hiyo ni kumvunjia heshima Juma Nature na kumfedhehesha huku akidai kuwa kwa heshima aliyonayo, hata yeye hawezi kufanya shoo hata kwa Tsh milioni moja.

"Wasafi hawawezi hata kunisogelea wakanitajia kiasi hicho finyu tofauti na heshima yangu," amesema 20-Percent.

Aidha, 20-Percent amesema walimuogopa ndiyo maana hawakuthubutu kumshirikisha. Amesisitiza hawezi kutaja kiasi anachotakiwa kulipwa kwenye shoo lakini siyo Tsh laki tano wala Tsh milioni moja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live