Kuna siku wapopo (wa Nigeria) watatutoa damu maana kila siku wanatupa stori mpya.
Wiki 3 zilizopita nilipiga stori na Jay Willz msanii wa Nigeria aliyeshirikishwa na #DiamondPlatnumz kwenye wimbo wa “Melody” alisema wasanii wengi wa Tanzania wana Melodies nzuri tofauti na Nigeria akiwa na maana ni rahisi kutengeneza muziki mzuri na watofauti.
Tukiachana na Jay willz wiki, nilipiga stori na Teni The Entertainer na yeye amewahi kushirikishwa na #DiamondPlatnumz kwenye wimbo wa “The Sound” na yeye akasema kitu kile kile anapenda sana muziki wa Tanzania kwa sababu ya Melody za wasanii wetu zipo tofauti na wasanii wa mataifa mengine.
Teni akatolea mfano kabisa anapenda Melody za Harmonize na Rayvanny pia aliweka wazi mipango yake ya kufanya kazi na wasanii wa Tanzania mwaka 2024.
Ukiachana na Teni na huyo Jay willz wapo wasanii wengi sana wa nje wamewahi kuweka wazi mapenzi yao kwa wasanii wa Tanzania kwa sababu ya Melody na lugha ya kiswahili ila cha ajabu wasanii wetu wengi hawafanyi vizuri kimataifa kupitia hizo Melody na Lugha ya kiswahili kama wenzetu wanavofanya vizuri kupitia melody zao na Lugha zao.
Ni kwamba wapopo wanatudanganyaga kutuambia lugha yetu ya kiswahili na melody za wasanii wetu wa Tanzania ni nzuri kumbe ni mbaya ndio maana tunakuwa na wasanii wachache wanaofanya vizuri kimataifa au wasanii wetu hawajui namna ya kutumia vizuri Lugha yetu ya Kiswahili na Melody zetu kutoboa kimataifa?