Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wapo wasanii wanatoa nyimbo tisa zinakataa ila sio kwangu – Bill Nass

3599 27878998 540540993011279 8080552067694854144 N 1 E1519112631312 TZW

Mon, 26 Feb 2018 Chanzo: bongo5.com

Msanii wa muziki Bongo, Bill Nass amefunguka kuhusu ukimya wake katika game.



Rapper huyo amejibu tetesi zinazoeleza kuwa ameshuka kimuziki baada ya Petty Man kuondoka katika label ya LFLG, Bill Nass ameiambia EATV kuwa hilo halina ukweli wowote.

“Huwezi kuzungumzia kushuka au kupanda kwa sababu bado sijatoa wimbo na fan base yangu ni ile ile angalau ningekuwa nimetoa nyimbo zinakataa,” amesema Bill Nass.

“Watu wanatoa nyimbo hata saba, nane, tisa zinakataa mimi sijatoa hata wimbo mmoja ukakataa kwa hiyo bado naamini material ambayo ninayo ni mengi,” amesisitiza.

Tangu kuanza kwa mwaka huu Bill Nass hajatoa wimbo hata mmoja zaidi ya kushirikishwa katika ngoma ya Rosa Ree ‘Marathon’. Ngoma yake ya mwisho kutoa ni ‘Sina Jambo’ iliyotoka Augost mwaka jana.

Chanzo: bongo5.com