Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

SIL

Waparamia ukuta wa shule kupeleka majibu ya Mtihani kwa ndugu zao

Waparamia Ukuta Waparamia ukuta wa shule kupeleka majibu ya Mtihani kwa ndugu zao

Tue, 12 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Marafiki, ndugu na wazazi wa wanafunzi wa darasa la 10 waliokuwa wakifanya mtihani muhimu katika shule ya Chandrawati huko nchini India Jumatano iliyopita, walifumwa wakiparamia kuta za shule hiyo ili kupitishi karatasi za majibu ya mitihani kwa wapendwa wao.

Shule hiyo hivi majuzi imejikuta kwenye kashfa kubwa ya udanganyifu wa mitihani baada ya video za watu wakipanda ukuta wa shule hiyo ili kuwapitishia wanafunzi majibu ya mtihani kuenea kwenye mitandao ya kijamii.

Maafisa wa shule hiyo waliohojiwa wanasema hakuna udanganyifu wowote uliotokea bali watu hao walijaribu tu kusaidia marafiki na jamaa zao bila mafanikio.

Gazeti la India Times linaripoti kwamba kuna mtu wa ndani alipiga picha ya karatasi ya mtihani shuleni hapo na kuwatumia ndugu wa wanafunzi waliokuwa nje ya shule, ambao walitafuta majibu na kuyaandika kwenye vipande vya karatasi, na kisha kuyapeleka kwa wanafunzi kupitia madirishani.

Mojawapo ya video hizo inawaonyesha watu waliopanda ukuta wakiwaita wanafunzi madirishani ili waweze kuwagawia majibu.

Hata hivyo licha ya ushahidi kuenea kwenye mitandao ya kijamii, maafisa wa shule wanajitetea kuwa video hiyo inaonyesha tu jaribio la udanganyifu, na kuongeza kuwa usalama ulikuwa mkali na hakuna chochote kilichoweza kuingia shuleni hapo kupitia madirishani wakati wa mtihani ulipokuwa ukiendelea.

"Kuna watu waliokuwa wakileta fujo tu nje ya shule lakini hakuna udanganyifu wowote uliofanyika ndani....ingawa walikuwa wakijaribu kuwaita wanafunzi waliokuwa ndani, tulihakikisha kwamba hakuna chochote kibaya kilichotokea," wahudumu wa shule walisema katika taarifa yao.

Licha ya kukana kabisa kwa maafisa wa shule, baadhi ya mashuhuda walisema udanganyifu ni tabia ya kawaida shuleni hapo.

“Hili ni jambo la kila mwaka, na nimekuwa nikishuhudia mara kwa mara” mwanafunzi wa zamani katika Shule ya Chandrawati aliliambia gazeti la Indian Express.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live