Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanenguaji wadaiwa ‘kuwateka’ wanaokwenda maonyesho

Tue, 10 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mbali na kuzuiliwa ndani ya viwanja vya maonyesho, muziki umeendelea kupigwa jambo ambalo limekuwa likisababisha wananchi wengi kuishia kwenye mabanda ya muziki badala ya kwenda kuangalia bidhaa mbalimbali.

Muziki hupigwa maeneo mbalimbali ya mabanda hayo, huku watu wakishindana kucheza kuvuta watazamaji.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi wamelalamikia kitendo hicho, huku wakidai muziki huo unapoteza ladha ya maonyesho kwani watu wanaangalia wanenguaji badala ya kutembelea mabanda ya bidhaa.

Akizungumzia suala hilo, ofisa uhusiano wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (Tantrade), Theresa Chilambo alisema kupiga muziki mkubwa eneo la mkusanyiko wa watu ni kosa kisheria na wameweka matangazo.

“Hatujapokea malalamiko kutoka kwa wananchi ila akijitokeza tutachukua hatua kwa mhusika, ikiwamo kumfungia huduma zake ndani ya maonyesho,” alisema.

Kuhusu ufinyu wa mabanda, alisema yapo katika kiwango cha kimataifa.

Chanzo: mwananchi.co.tz