Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanawake wanamuziki watangaziwa neema

Wanawake wanamuziki watangaziwa neema

Sun, 10 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Katika kusherehekea siku ya wanawake duniani ‘App ya Boomplay’ itakuwa na kampeni kabambe ambayo itatoa fursa ya kukuza mauzo ya kazi za wanawake ambao nyimbo zao zitakuwepo kwenye playlist ya Boom Queens.

Boom Queens ni kampuni mpya ambayo imeanzishwa mwezi huu wa maadhimisho ya siku ya wanawake.

Mbali na hilo, pia App hiyo itakuwa na  mwonekano tofauti unaolenga kuonyesha na kukuza kazi za wanawake katika muziki kupitia kampeni yake mpya ya Boom Queen’

Boomplay ni ‘app’ kwa ajili ya huduma ya kusikiliza na kupakua muziki barani Afrika ambapo imeungana na wanawake duniani kote katika kusherehekea siku hii leo Ijumaa Machi 8, 2019.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa, Meneja Mahusiano wa kampuni ya Boomplay, Tosin Sorinola amesema mbali na kukuza mauzo ya wasanii pia watumiaji wa mtandao wa App hiyo wataweza kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo iPhone X.

“Majadiliano ya usawa wa kijinsia ni moja ya mambo ambayo ni muhimu kwetu kama jukwaa lenye nia kubwa ya kukuza wanawake katika muziki na kampeni hii itakuwa endelevu na hili litadhihirishwa katika shughuli zetu za kila siku,” amesema Sorinola.

“Vanessa Mdee, Rihanna, Tiwa Savage, Fena Gitu ni miongoni mwa wanawake wenye vipaji ambao wameendelea kuibadili tasnia ya muziki duniani,”

Amesema ili watumiaji kuweza kujishindia zawadi kupitia simu zao za android na iOS wanatakiwa kutumia vifurushi vinavyopatikana katika App ya Boomplay vya siku, wiki na mwezi pamoja na kusikiliza playlist ya Boom Queens.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz