Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Wanawake Watano DRC Waishtaki Ubelgiji

Wanawake 6 Wanawake Watano DRC Waishtaki Ubelgiji

Fri, 15 Oct 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Wanawake watano wenye asili ya Kongo na Ubelgiji, waliotengwa na familia zao wakati wa ukoloni wameishtaki serikali ya Ubelgiji kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu. Wanawake hao wanasema walichukuliwa kutoka kwa mama zao weusi wakati wa kuzaliwa tu kwa msingi wa rangi ya ngozi yao.

Wanawake hao watano walikuwa kati ya maelfu ya watoto waliochukuliwa kutoka kwa familia zao na kupelekwa kwenye vituo vya kulelea watoto vya kidini kwa kuwa lilikuwa ni agizo kwa wakati ule wa ukoloni.

Wengi wao walikuwa hata hawawafahamu baba zao wazungu. Wale ambao wameenda mahakamani hawakupelekwa Ubelgiji wakati Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo ilipopata uhuru mnamo 1960. Ubelgiji inashtakiwa kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu, kosa ambalo hakuna kikomo cha wakati.

Chanzo: globalpublishers.co.tz