Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanaume anaowapenda Zari wana sifa hizi 5

ZARI MAPENZI Zifahamu sifa 5 zinazomvutia Zari kwa mwanaume

Wed, 3 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku za hivi karibuni, mwanasoshalaiti wa Uganda, Zari Hassan amekuwa akionyesha wazi kuwa yupo kwenye mahusiano.

Bila wasiwasi, mama huyo wa watoto watano amekuwa akimwanikan mpenzi wake wa sasa ambaye ameibua gumzo kutokana na umri wake kuwa mdogo kuliko Zari jambo linazungumzwa kuwa imekuwa kawaida kwa Zari kutembea na vijana anaowazidi umri.

Hata hivyo tayari amewajibu wakosoaji wake kwa kuwaeleza kuwa uamuzi wa nani kuwa naye kimahaba ni jukumu lake na si walimwengu.

"Ukiniambia nichumbie nani na nisichumbie nani, nawajua wa aina hizo. Lakini hapa ndipo ninapoamua kubaki. Ni nini kinachokufanya ufikiri kwamba watu wengine hawana hadhi?

"Niko hapa kwa sababu nataka kuwa hapa, sio kwa sababu mnataka kunichagulia mahali pa kuwa," alisema Zari hivi karibuni.

Wapenzi wa Zari wa zamani ambao wanajulikana wameonekana kuwa na sifa sawa au zinazokaribiana sana.

Sifa hizi ni pamoja na:-

1. Ni wadogo kuliko yeye

Wapenzi wengi wa zamani wa mwanasoshalaiti huyo wanaojulikana wamebainika kuwa na umri mdogo kuliko yeye.

Hawa ni pamoja na Diamond Platnumz ambaye ni mdogo wake kwa takriban miaka kumi, King Bae, GK Choppa, Dark Stallion na mpenzi wake wa sasa.

Aliyekuwa mume wake, marehemu Ivan Semwanga hata hivyo alikuwa amemzidi umri kwa miaka mitatu.

2. Ni wenye misuli

Ni wazi kuwa akriban wanaume wote ambao wanajulika kuwahi kuwa kwenye mahusiano na mwanasoshalaiti huyo wamejenga misuli kweli.

Zari ameonekana kuvutiwa zaidi na wanaume wanaopenda kufanya mazoezi na wenye misuli minene.

Mara nyingi mwanasoshalaiti huyo pia ameonekana kuvutiwa zaidi na wanaume warefu.

3. Wenye ngozi ya chokoleti

Wapenzi wengi wa zamani wa Zari wameonekana kuwa na ngozi yenye rangi nyeusi na mguso kidogo wa kahawia.

Hawa ni pamoja na marehemu Ivan, Diamond, Dark Stallion, GK Choppa na mpenzi wake wa sasa

4. Wachapa kazi

Zari Hassan ameonekana kuvutiwa zaidi na wanaume wenye bidii kubwa na malengo makubwa ya kimaisha.

Ingawa sio maelezo ya kazi ya wapenzi wake wote ambayo yapo wazi, yale yanayojulikana yamedokeza kuwa Zari anapendelea wanaume wanaojituma zaidi maishani.

Marehemu Ivan Semwanga alikuwa mfanyibiashara mkubwa, sawa na GK Choppa na Diamond Platnumz ambaye ni msanii mkubwa Afrika na tajiri.

5. Wapenda anasa

Wapenzi wengi wa Zari wamebainika kuwa watu wasiojifungia na wanaopenda burudani za aina tofauti tofauti.

Zari ambaye pia ni wazi anapenda raha ameonekana mara nyingi akijivinjari na wanaume anaochumbiana nao katika maeneo ya burudani.

Akizungumza hivi majuzi, Zari alitangaza kuwa maisha yake hayafungwi na sheria zilizowekwa na jamii. Mwanasoshalaiti huyo alibainisha kuwa ana haki ya kumchagua yule ambaye angependa kuchumbiana naye.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live