Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Wanaochangia 'earphone' hatarini kupata fangasi za masikio

Wanaochangia 'earphone' Hatarini Kupata Fangasi Za Masikio Wanaochangia 'earphone' hatarini kupata fangasi za masikio

Thu, 25 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kutokana na maendeleo ya teknolojia, kumekuwa na uzalishaji wa vitu vingi vyenye kurahisisha maisha ambavyo awali havikuwepo, huku wataalamu wa masuala hayo wakiendelea kubuni vitu vipya kila kukicha.

Hapo awali watu walisikiliza muziki kwa kutumia simu zao wakiwa wamezishika mkononi, huku sauti ya kinachosikilizwa ikisikika kwa kila mtu.

Kutokana na maendeleo ya teknolojia, kwa sasa ni nadra kukutana nalo kwani wengi hutumia vifaa mbalimbali vijulikanavyo kama spika za masikioni (earphone, head phone na ear pod) kwa ajili ya kuzuia sauti ya wanachosikiliza isisikike kwa watu wengine.

Katika matumizi ya vifaa hivyo kila mtu huwa na sababu zake, huku kukiwa na wale wanaodai kuwa hulazimika kutumia kwa ajili ya kutosumbua wengine.

Licha ya mazuri hayo yote, jambo lililozoeleka miongoni mwa watu hasa wanaokaa pamoja muda mwingi ikiwemo vyuoni, maofisini na katika shughuli mbalimbali ni kuazimana hivi vifaa vya masikioni.

Mkuu wa Kitengo cha Masikio, Pua na Koo, Dk Bukanu Faustine kutoka hospital ya Benjamin Mkapa, jijini Dodoma amesema wengi huazimana bila kujali afya za masikio ya yule anaye muazima, hali ambayo humfanya kuyaweka rehani masikio yake.

"Kwa watu wanaopenda kuazimana vifaa hivyo, wapo kwenye hatari kubwa ya kuambukizana ugonjwa wa fangasi kwenye masikio," amesema Dk Banaku. Kasome zaidi kwenye website ya mwananchi scoop link kwenye bio.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live