Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Wanandoa wanaotaka kujiua waongezeka

Sarco Euthanasia Pod Sw Wanandoa wanaotaka kujiua waongezeka

Thu, 12 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Picha za kwanza za vifaa vya kusaidia Watu kufa “Sarco Euthanasia Pod” vitakavyotumika katika shughuli ya kutoa uhai wa Wanandoa wawili wa Uingereza zimeoneshwa rasmi hadharani na Kampuni ya The Last Resort ambayo itaifanya shughuli hiyo.

Peter na Christine Scott ambao wameoana kwa miaka 46, walithibitisha wiki hii kwamba wamefanya uamuzi wa kukatisha maisha yao kwa wakati mmoja kwenye vifaa hivyo baada ya mmoja wao kugundulika hivi karibuni kuwa na ugonjwa wa shida ya akili.

Wanandoa hao wenye umri wa miaka 80 na 86 ambao wana Wajukuu sita, sasa wanatarajiwa kuwa Wanandoa wa kwanza kondoa uhai wao kupitia vifaa vya The Last Resort, Shirika lenye Makao yake Makuu Nchini Uswizi ambalo linatoa msaada wa Watu kufa bila tabu katika kifaa chake kiitwacho Sarco kilichozinduliwa Julai 2024.

Sanduku hilo la Watu wawili litatengenezwa kwa kutumia kichapishi cha 3D na litakuwa na kitufe kimoja au viwili ambavyo Wakaaji wanaweza kubonyeza ili kusababisha vifo vyao ambapo hadi sasa rekodi zimeonesha kuwa tayari Watu 120 wameomba kukatisha uhai wao kupitia kifaa hicho ambapo wengi ni Raia wa Uingereza kwa mujibu wa The Last Resort.

Kifaa hicho hufanya kazi kwa kubadilisha hewa kwa asilimia 100 ya Nitrojeni na kumfanya Mtu aliyepo ndani yake kupoteza fahamu na kushindwa kupumua ndani ya dakika chache, amesema Philip Nitschke, Mvumbuzi wake ambaye amepewa jina la Daktari wa Kifo.

Kufa kwa kusaidiwa ni kinyume cha sheria Nchini Uingereza lakini Wanandoa hao walisema wiki hii kwamba wanataka kushiriki hadithi yao pamoja ili kuongeza uzito wa hoja zao kuhalalishwa na Serikali ya Nchi hiyo kutokana na uwepo wa Wanandoa wengine ambao tayari wamewasilisha maombi kama hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live