Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Wanandoa waliofuga paka 159 wapigwa marufuku kufuga wanyama tena

Wanandoa Wa Ufaransa Waliofuga Paka 159 Wapigwa Marufuku Kufuga Wanyama Tena Wanandoa waliofuga paka 159 wapigwa marufuku kufuga wanyama tena

Thu, 4 Apr 2024 Chanzo: Bbc

Wanandoa wa Ufaransa wamehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja kwa kuwaweka wanyama kadhaa katika mazingira ya ukatili.

Wanandoa hao, kutoka Nice, walikuwa wamefuga paka 159 na mbwa saba katika gorofa yao ya ukubwa wa 80sqm (861sqft).

Wanyama waligunduliwa mwaka jana wakiishi katika mazingira ya uchafu, wengi wakiwa wamepungukiwa na maji, wakikabiliwa na utapiamlo au kuambukizwa vimelea.

Hakimu alisema wanandoa hao walikosa kuwatunza wanyama hao ipasavyo.

Wanandoa hao, mwanamke, 68, na mwanamume mwenye umri wa miaka 52, pia walipewa marufuku ya kudumu ya kufuga wanyama nyumbani.

Waliamriwa kulipa zaidi ya €150,000 (£128,000) kwa mashirika ya misaada ya haki za wanyama na vyama vya kiraia.

Mwaka jana, polisi waliingia katika nyumba ya wanandoa hao na kugundua makumi ya wanyama katika kila chumba.

Mamlaka ziliripoti uwepo wa kinyesi cha wanyama kila mahali.

Baadhi ya paka na mbwa hao walikufa kwa sababu ya afya mbaya.

Wachunguzi walipata miili ya paka wawili na mbwa wawili katika bafuni.

Mmiliki wa orofa hiyo aliiambia mahakama kwamba wanyama hao walikuwa "kipenzi cha maisha yake" lakini kwamba alikuwa "amezidiwa na malezi".

Inaonekana alikuwa amechukua paka watatu na mbwa watatu wa wazazi wake mnamo 2018, kabla ya kuleta karibu paka 30 wanaoishi katika jengo lililotelekezwa kwenye gorofa yake. Wanyama hawa baadaye walizaana.

Chanzo: Bbc