Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanandoa wafunga kula, kunywa kwa siku 4

Maombi Jr Wanandoa wafunga kula, kunywa kwa siku 4

Sat, 8 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwenye ulimwengu wa sasa wanaume wengi huwa na matakwa ambayo huazimia kupata kwa wapenzi wao kabla ya kuazisha safari ya miaka ya raha na karaha kwenye ndoa.

Kuna wanaoonelea kupata mchumba mwenye umbile unaovutia ni sawa na wengine kusema mwanamke ni yule mnyenyekevu na mcha Mungu.

Kwenye video inayosaamba kwenye mtandao wa TikTok inaonyesha wanandoa wawili walioafikiana kutenga siku kadhaa kifunga kula na kunywa ili kufanya sala la maombi.

Mwanamke huyo anayejuliakana kama Yvonne alienda mlimani na mumewe kusali kwa siku nne mfululizo kuombea mahitaji yao ya kindoa.

Video hii iliwafanya watumizi wa mitandao kuwapongeza wapenzi na wengine kusema kitendo hicho ni cha kuigwa na cha kielelezo. Ila kunao baadhi ya watumiaji walitumia nafasi hiyo kuonyesha kutorithishwa na maamuzi ya wanandoa hao.

"Hii ni njia nzuri sana ningependezwa iwapo ningepata mwanaume kama huyo." Mmoja wa wa shabiki alisema.

"Si kila kitu unatia kwenye mtandao. Haya ni mambo ya familia yako na Mungu. Mungu akubariki." Mwingine aliongeza.

"Mungu akujibu maombi...Naomba pia anipe mtu ambaye tunaweza kuutafuta uso wake pamoja..." Shabikia anayejiita Shii alisema.

"Hautakosa familia ambayo kuomba pamoja itashinda daima. Timo Austin alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live