Huko nchini Uganda Kenneth na Christine wamethibitisha kwamba upendo hauna mipaka na upendo wa kweli unaweza kushinda kizuizi chochote hii ni kutokana na uhusiano wao wa umbali mrefu ulivyokua na baadaye kuwa ndoa.
Safari yao imekuwa na kila ishara ya matumaini kwa wengine, ikidhihirisha nguvu ya upendo licha ya kukabiliwa na kukatishwa tamaa na watu wengine, hasa kutokana na tofauti za kikabila, wapenzi hao walibaki imara na wasioathiriwa na jambo lolote nje ya uhusiano wao, walipuuza mawazo hasi na kuendeleza uhusiano wao kwa kuwasiliana mara kwa mara.
Ukaribu wao ulizidi kuimarishwa walipoamua kuomba shauri mbalimbali kutoka kwa watalaamu wa mahusiano na ndoa. Uzoefu huu ulithibitisha imani yao ya kujiepusha na uhusiano wa kimwili mpaka ndoa.
Kujitolea kwao kwa uamuzi huu wa kutoshiriki tendo la ndoa kabla ya ndoa ulikuwa imara, kwani walithamini uhusiano wao. Kenneth aliiambia chombo cha habari cha Monitor:
"Tulichagua ndoa takatifu na tukajitolea kujiepusha na ngono mpaka ndoa. Ndoa ni nzuri, hasa ikiwa unafuata uaminifu na uadilifu. Oa ukiwa kijana na mwenye nguvu."
Siku yao ya harusi ilikuwa ya kuvutia, ikihamasisha watu wengi, hasa wale ambao wanaendelea kujiepusha kukutana kimwili hadi ndoa.