Wanafunzi wanojiunga na vyuo mbalimbali nchini wametakiwa kujiepusha na vishawishi ikiwemo kujiingiza kwenye makundi yasiyofaa pamoja na kujiingiza kwenye mahusino ya kimapenzi wawapo vyuoni vinavyopelekea kukatisha ndoto zao.
Kauli hiyo imetolewa jijini Mwanza na Mkurugenzi wa shirika la kutetea haki za wanawake na watoto la Kivulini Yassin Ally, wakati anawajengea uwezo wa kujitambua wanafunzi wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), kampasi ya Mwanza ndipo akawataka kujiepusha na vishawishi na badala yake wazingatie kilichowapeleka chuoni hapo
"Rai yangu ni kwa wanafunzi wote wanojiunga kwa mwaka wa kwanza nchi nzima ni kwamba wanapofika vyuoni waelewe uhuru huu usiokuwa na mipaka wasiposimamia malengo yao wakajitambua, wataangukia kwenye matapeli wa mapenzi ama kwa wanafunzi wenzao ama siyo wanafunzi na zinaathari sana kwenye malengo yao," amesema Ally
Kwa upande wake Naibu Kamishna wa Jinsia na Maendelo ya Wanawake vyuoni TAHLISO Hawa Issa, akawasisitizia wanafunzi wa vyuo kuishi maisha yao na kuacha kuiga vitu visivyofaa.