Makala ya filamu ya Netflix ambayo inaonyesha Malkia Cleopatra VII kama Mwafrika mweusi imezua gumzo nchini Misri.
Mwanasheria amewasilisha malalamiko yanayowashutumu African Queens kuwa Malkia Cleopatra amekiuka sheria za vyombo vya habari na kulenga "kufuta utambulisho wa Misri".
Mwanaakiolojia mkuu alisisitiza kuwa Cleopatra alikuwa "na ngozi nyeupe, sio mweusi".
Lakini mtayarishaji huyo alisema "urithi wake unajadiliwa sana" na mwigizaji anayecheza naye aliwaambia wakosoaji: "Ikiwa hupendi maigiza, usitazame kipindi hicho."
Adele James alitoa maoni hayo katika kurasa ya Twitter iliyoangazia picha za maoni ya matusi ambayo yalijumuisha matusi ya kibaguzi.
Cleopatra alizaliwa katika jiji la Alexandria nchini Misri mwaka 69 KK na akawa malkia wa mwisho ya watu wanaozungumza Kigiriki iliyoanzishwa na jenerali wa Alexander the Great wa Macedonia Ptolemy.
Alimrithi baba yake Ptolemy XII mwaka 51 KK na kutawala hadi kifo chake mwaka 30 KK.
Baadaye, Misri ilianguka chini ya utawala wa Warumi.
Utambulisho wa mama yake Cleopatra haujulikani na wanahistoria wanasema inawezekana kwamba yeye, au mtu mwingine wa kale wa kike, alikuwa Mmisri wa kiasili au kutoka kwingineko barani Afrika.
Tovuti shirikishi ya Netflix ya Tudum iliripoti mnamo Februari kwamba chaguo la kumuigiza Adele James, mwigizaji wa Uingereza ambaye ni wa kabila mchanganyiko, kama Cleopatra katika filamu yake mpya ilikuwa "kuashiria kwa mazungumzo ya karne nyingi kuhusu mtawala".
Jada Pinkett Smith, muigizaji wa Marekani ambaye alikuwa mtayarishaji mkuu na msimulizi, alinukuliwa akisema: "Si mara nyingi tunapata kuona au kusikia hadithi kuhusu malkia weusi na hiyo ilikuwa muhimu sana kwangu na kwa binti yangu na kwa jamii yangu tu kuweza kujua hadithi hizo kwa sababu zipo nyingi!"
Lakini tangazo la filamu hiyo ilipotolewa wiki iliyopita Wamisri wengi walikasirishwa na taswira ya Cleopatra.