Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wamekimbilia ughaibuni buana!

Ughaibuni Pic Data Wamekimbilia ughaibuni buana!

Sat, 10 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

TANZANIA imejaaliwa kuwa na wasanii wengi ambao kwa namna moja au nyingine wamekuwa na mchango katika ukuaji wa sanaa.

Ni kutokana na kupatta umaarufu baahi ya wasanii wamejikuta wakipata michongo ya kwenda nje ya nchi na wengine wakijikuta wanalowea huko mazima.

Katika makala haya yanawaangazia kati yao na kwa wachache kueleza nini wanafanya huko.

Charles Magari

Unamkumbuka mzee mtata katika tamthilia mbalimbali zilizochezwa na kundi la Kaole na kwenye filamu ya Red Valentine na nyiginezo?

Related SUPASTAA UTAMUELEZA NINI WEWE!Huyu sio mwingine bali ni Charles Magari, maarufu kwa jina la Mzee Magari. Basi unaambiwa kwa sasa mzee huyu yupo zake nchini Marekani.

Kwa mujibu wa rafiki yake wa karibu Hashim Kambi, ambaye naye ni msanii anasema Magari alijikuta akilowea huko mwaka 2015 baada ya wao kupata mualiko.

Anasema mualiko huo pamoja na wenzake waliupata kutoka kwa Mtanzania anayeishi nchini humo kwenda kucheza filamu iliyopewa jina la ‘Dar to Washington DC.

“Nakumbuka ilikuwa mwaka 2015 wakati hayati John Magufuli anaingia madarakani, hapo ndipo tukapata mualiko na wenzangu kwenda kucheza filamu nchini Marekani, ninashukuru tuliimaliza kazi hiyo salama,” anasema.

Hata hivyo, anaeleza baada ya kufanya kazi hiyo alikaa huko kwa takribani miaka nane lakini maisha yalimshinda na kuamua kurudi zake nyumbani.

Wakati Kambi akifanya hivyo, wenzake Frank na Magari waliamua kuanzisha maisha yao mapya ambapo Magari sasa hivi ameoa na ana mtoto huko.

“Kwa ukaribu ambao niko na familia ya Magari amekuwa akiniagiza kwenda kuwaona watoto wake ambao wapo hapa nchini kwani mama yao alishafariki tangu mwaka 2008,” anasema.

Akielezea sababu ya yeye kutoona haja ya kuendelea na maisha nchini Marekani, Kambi anasema alijikuta tu akishindwa kuendana na maisha ya huko huku mara nyingi akipakumbuka nyumbani na ndio maana aliamua kurejea na kuwaacha wenzake huko japo anabainisha siku aliyoondoka walilia sana.

Frank

Kama kambi alivyoelezea hapo juu, kwamba mualiko wa Marekani waliupata yeye, Magari na Frank.

Hivyo Frank ambaye jina lake halisi ni Mohamed Mwikongi, naye aliamua kubaki huko.

Hata hivyo, anasema Frank tofauti na Magari ambaye ameamua kutengeneza familia huko, yeye huko anasaka tu maisha lakini familia yake ikiwemo mke wake wapo hapa nyumbani Tanzania.

Hata hivyo, mwaka 2015, msanii huyo alikuja nchini na kutangaza azma ya kuwania ubunge Jimbo la Segerea kupitia chama cha ACT Wazalendo, lakini bahati haikuwa yake kwani ushindi ulikwenda kwa Bonnah Kamoli kupitia chama cha Mapinduzi(CCM).

Dayna Nyange

‘Nivute Kwako’ ndio kibao kilichomtoa kwa mara ya kwanza kwenye muziki wa Bongofleva. Kwa sasa Dayna Nyange japo hajaacha kabisa kazi hiyo, anafanya shughuli zake nchi Afrika Kusini ikiwemo biashara ambazo hakuwa wazi kutaja ni aina gani ya biashara anafanya alipozungumza na Mwanaspoti.

“Kule Afrika Kusini najishughulisha pia na biashara, lakini ni biashara gani bado ipo chini ya kapeti ila siku moja mtakuja kujua,” anasema Dayna.

Licha ya kupotea kwa muda mrefu miaka miwili ya hivi karibuni amekuwa akija nchini mara kwa mara na kuonekana katika matukio mbalimbali ya burudani.

Irene Sanga

Ni kati ya watu waliomfundisha mghani wa mashairi Mrisho Mpoto.

Tangu alipomtungia kibao cha Salamu Zako Mjomba, Mpoto amekuwa moto wa kuo-tea mbali kwani licha ya jina lake kuwa Mrisho Mpoto, watu wanamfahamu zaidi kwa jina la Mjomba na kuwa kati ya waanii wanaoheshimika.

Irene ambaye alichangia umaarufu wake huo kwa sasa anaishi nchini Uholanzi, ambapo anaendelea na shughuli zake za sanaa za majukwaani ambazo anaeleza huko wanazithamini na zinalipa kuliko hapa.

Ni katika ujuzi wake huo, hivi karibuni anatarajiwa kuwa miongoni mwa waongozaji wa filamu itakayoongozwa na waongozaji kutoka nchi 100 duniani kupitia mtandao.

Ray C

Huyu kwa sasa yupo nchini Ufaransa. Licha ya kuonekana kuendelea na muziki tangu alipopitia matatizo ya utumiaji dawa za kulevya, haijajulikana haswa anafanya nini huko.

Fresh Jumbe

Mkali huyu wa wimbo wa ‘Penzi ni Kikohozi’ anafikisha miaka 25 tangu atimkie nchini Japan.

Jumbe anasema kuwepo kwake huko ni kwa ajili ya shughuli zake za muziki na sasa anamiliki bendi yake inayoitwa ‘African Express’

“Ni kweli muda mrefu nipo nchini Japan, lakini Tanzania ni nyumbani hivyo naamini ipo siku nitarudi tu japo sijui ni siku gani haswa nitarudi,” anasema.

Wengine wanaioshi ughabuni ni pamoja na Wabogojo Ford (China), Balozi Dola Soul (Marekani) Cloud 112, Lucy Komba, Ige Moyaba, Jesca Charles na wengine wengi.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz