Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wamefika pabaya! Barakah The Prince amtolea amtukana Kiba hadharani

Baraka Kiba Nm.jpeg Wamefika pabaya! Barakah The Prince amtolea amtukana Kiba hadharani

Sat, 3 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva, Barakah The Prince ni kama ametoa kile kilichokuwa kinamsibu moyoni mwake kwa kipindi kirefu baada ya kuzungumza na moja ya vyombo vya habari.

Barakah ambaye amekuwa akimponda Kiba tangu msanii huyo kutoka Rock City alivyojiondoa kwenye lebo ya Rock Star, amesema hamkubali kabisa na hampendi msanii mwenzake wa Bongo Fleva, Alikiba ambaye aliwahi kuwa naye kwenye lebo moja.

Barakah amebainisha hilo baada kuulizwa kwanini aligoma kutumbuiza wimbo ambao ni kolabo yake na Alikiba uitwao #Nisamehe, wimbo uliotoka mwaka 2017, ikiwa mashabiki walihitaji auimbe wimbo huo jukwaani kwenye show yake aliyoifanya usiku wa leo huko Jijini Mwanza lakini Badala yake aliwajibu kwa Kusema "Ali kiba ni mpu****vu" (tusi).

Pia Barakah kwenye mahojiano hayo ameendelea kwa kusema kwamba hii ni biashara na haitotokea shabiki wa Simba akiisifia Yanga au wa Yanga akaisifia Simba na shabiki wa Man United akiisifia Liverpool.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live