Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliomuua Eva wahukumiwa kunyongwa hadi kufa

Screenshot 2021 11 27 At 11.56.08 660x400.png Waliomuua Eva wahukumiwa kunyongwa hadi kufa

Sat, 27 Nov 2021 Chanzo: millardayo

Mahakama Kuu Kanda ya Iringa iliyokaa kupitia kikao chake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Njombe, imewahukumu Washtakiwa wawili Mwapulise Mfikwa (29) na Manase Mhada (25) kunyongwa hadi kufa kutokana na kukutwa na hatia ya kumuua Eva Merikion Mgaya (28) nyumbani kwake katika kijiji cha Ihanga wilayani Njombe.

Washtakiwa wao walitekeleza mauaji hayo baada ya kuvamia nyumbani kwa Eva walipofika kwa lengo la kuiba, akisoma hukumu hiyo Jaji Filmin Matogolo amesema tukio la mauaji lilitokea May 08, 2015 baada ya wawili hao kwenda nyumbani kwa Wilfred Vitus Ng’olo ambaye ni Mume wa marehemu wakiwa na bunduki iliyotengenezwa kwa njia za kienyeji ambapo walivamia, kuiba na kunyang’anya fedha .

Washtakiwa hao pia walichukua simu ya Mume wa marehemu na kumpiga risasi Eva Merikion Mgaya kifuani kwa kutumia bunduki hiyo na kusababisha kifo chake papohapo na kisha kutoweka mpaka walipokuja kukamatwa baada ya upelelezi juu ya mauaji hayo.

Chanzo: millardayo