Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliochemka kwa vigogo wageuka lulu Ligi Kuu

Yondan Polisi Pic Data Waliochemka kwa vigogo wageuka lulu Ligi Kuu

Sat, 9 Jan 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Charles AbelMore by this Author Dar es Salaam. Wakati zikibaki siku 12 kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa, wachezaji walioachwa na wale wanaosotea benchi katika timu za Azam, Simba na Yanga wameonekana kugeuka lulu katika timu nyingine.

Klabu mbalimbali zinazoshiriki Ligi Kuu msimu huu zimeonekana kuwachangamkia wachezaji hao kwa kuwasajili moja kwa moja na wengine kwa mkopo wakiamini wataimarisha vikosi vyao.

Na katika kuthibitisha hilo, kundi kubwa la wachezaji hao wameingia moja kwa moja katika vikosi vya kwanza vya timu hizo ambazo baadhi bado zinahaha kujiondoa katika mstari wa kushuka daraja kwenye msimamo wa ligi hiyo msimu huu.

Ihefu inayoshika mkia katika msimamo wa Ligi na pointi zake 13, yenyewe imeonekana kutowalazia damu wachezaji wa mkopo ama walioachwa na timu hizo tatu kubwa nchini ambao wengi wameingia katika kikosi cha kwanza.

Timu hiyo ya Mbeya imewasajili Joseph Mahundi aliyekuwa mchezaji huru baada ya kuachwa na Azam FC katika dirisha kubwa lakini pia imemsajili kwa mkopo winga Juma Mahadh kutoka Yanga ambao wote wapo katika kikosi cha kwanza na inaye kipa Deogratias Munishi aliyeidakia Lipuli FC msimu uliopita baada ya kuachana na Simba.

Timu ya Polisi Tanzania yenyewe tayari imewanasa kiungo Abdulaziz Makame wa Yanga na beki Kelvin Yondani. Makame amesajili kwa uhamisho wa mkopo wakati Yondani amesajiliwa moja kwa moja kama mchezaji huru kwani hakuwa na timu tangu alipoachana na Yanga.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz