Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walichosema mastaa wa kike baada ya Samia Suluhu kuapishwa kuwa Rais

Samiauraisipic Data Walichosema mastaa wa kike baada ya Samia Suluhu kuapishwa kuwa Rais

Fri, 19 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Aliyekuwa Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, ameapishwa rasmi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hafla ya kuapishwa kwake imefanyika leo Ijumaa Machi 19, 2021, Ikulu Dar es Salaam na kuweka historia ya kuwa rais wa kwanza mwanamke nchini Tanzania.

Samia amechukua nafasi ya aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, 2021 kwa maradhi ya moyo katika hospitali ya Mzena alikokuwa akipatiwa matibabu.

Baada ya uapisho huo mastaa mbalimbali wa kike wametoa na pongezi akiwemo msanii wa filamu, Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu ambaye kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram aliweka picha ya kiongozi huyo akiwa anaapa na kuandika’Madam President, Mungu Ibariki Tanzania,”.



Kwa upande wake mrembo Wema Sepetu ameaandika” Mama Samia wangu mimi. Sasa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wow...??????,”.

Naye Jacqueline Mengi, aliyewahi   kuwa Miss Tanzania mwaka 2000, ameandika “Japo bado tumegubikwa na wingu la huzuni, tunapata faraja kwa uwepo wako. Nafasi hii mpya unayochukua unaimudu sana, sio tu kama mama au mwanamke lakini ni kwa busara,utu, utulivu na ushupavu uliobarikiwa nao.



“Mungu akutangulie na akuongoze, kazi hii ni nzito na imejaa lawama maana kama kiongozi wa nchi huwezi kumfurahisha kila mtu. Kila la heri Mama Samia Suluhu Hassan tunakuamini na tunakupenda.

Rrita Paulsen, yeye ameandika”Mheshimiwa Mheshimiwa Rais Samia_Suluhu_Hassan, hii ni historia ya wakati gani,”.

Aliyewahi kuwa Miss Tanzania mwaka 1999, Hoyce Temu, ameanmdika”Kila la kheri Rais wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan na Mungu ailaze roho ya Marehemu baba yetu John Magufuli mahala pema peponi, Tanzania inahuzunuka,”.

Shufaa Rutiginga , ambaye mama wa mwanamitindo, Hamisa Mobetto, ameandika”Mungu ibariki Tanzania na rais wetu.Ni siku mpya kwa Tanzania.Mungu akubariki na akufanyie wepesi kwa kila jambo.Takbir.

Wakati muigizaji Yobnesh Yusuph , maarufu kwa jina la Batuli, ameandika “Madame President, Mheshimiwa  Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania,”.

Huku msanii Zuwena Mohamed, maarufu kwa jina la Shilole ameandika” Mungu akubariki mama na akuongoze vyema.Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki Rais wetu.

Msanii wa muziki wa Bongofleva, Mwasiti Almas yeye ameandika” Mama Samia tunakutakia kila heri. Tunakuombea busara, hekima na unyenyekevu katika kazi ya kuliongoza taifa letu! Mungu ibariki Tanzania,”.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz