Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walichokisema Lulu na Mama Kanumba baada ya kupatana

Ruto Msfgs Walichokisema Lulu na Mama Kanumba baada ya kupatana

Sun, 10 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa muda mrefu kumekuwa na mkanganyiko wa kutokuelewana kati Elizabeth Michael 'Lulu' na mama wa aliyekuwa Mwigizaji wa Filamu nchini Marehemu Steven Kanumba, Mama Kanumba. Ambapo chanzo cha ugomvi wao kilianza baada ya mama Kanumba kumtuhumu Lulu kuwa ndiye chanzo cha kifo cha mwanae Kanumba. Wote tuliona kuna kipindi walikuwa kwenye majibizano ambayo hayakuwa mazuri baadae wakatulia bila kuyamaliza hadi siku ya juzi walipokutana Arusha.

Hiki ndicho alichokizungumza Lulu baada ya kukutana na Mama Kanumba kwa mara ya kwanza.

"Tukio la kukutana na Mama Kanumba mimi nalifurahia, siyo jana tu nalifurahia mara zote na siku zote, tunashukuru Mungu kwa hapa tulipofika vitu vingine vyote ni vya kibinadamu yule ni mzazi simlaumu kwa chochote na kwa namna yoyote anayojisikia yeye kama mzazi ana haki ya kujisikia vyovyote anavyojisikia. Huu ni msalaba wangu Mungu alishanipa na utakuwa chini ya mabega yangu siku ambayo nitakuwa sipo duniani kwahiyo nitapambana nao kwa namna yoyote"

"Namshukuru Mungu mama yangu ana furaha sasa hivi ni jambo la kumshukuru Mungu, lakini simlaumu na sijawahi kujisikia vibaya kwa chochote. Binadamu tunavyokuwa tunaweka vitu moyoni tunajizuilia baraka zetu kwahiyo nimefurahi na naamini tutazidi kubarikiwa kwasababu tumefanya moja ya kitu ambacho Mungu anakipenda sana," amesema Lulu

Kwa upande wa mama Kanumba yeye amesema amefurahi sana na ameshindwa hata kula chakula baada ya kuwa Sawa na Lulu kisha kuongeza

"Mtoto akipotea akirudi mzazi lazima ufurahi, kwahiyo na mimi nimefurahi," amesema Mama Kanumba kisha akawazuia Waandishi wasiendelee kumuuliza maswali kuhusu Lulu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live