Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakwe wamkataa Kanye West

Kanye West And Bianca Censori Are Seen On May 13 2023 In News Photo 1694888568 Wakwe wamkataa Kanye West

Mon, 20 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

‘Rapa’ kutoka nchini Marekani, Kanye West anadaiwa kutengana na mkewe Bianca Censori baada ya familia ya Bianca kuomba mrembo huyo aachane na Kanye kutokana na tabia zake.

Familia ya Bianca imekuwa ikilalamika jinsi Kanye anavyoishi na mrembo huyo ambapo baada ya kuolewa tu Bianca maisha yake yalibadilika muonekano na hata mavazi jambo ambalo familia yake hawakubaliani nalo.

Kwa mujibu wa Daily Mail inaeleza kuwa marafiki na familia ya Bianca kwa pamoja wamekuwa wakimlazimisha amuache Kanye na adai talaka kwani amekuwa akimpangia hadi vyakula vya kula.

Kanye mwenye umri wa miaka 46 alimuoa Bianca Disemba 2022, mwezi mmoja tu baada ya taratibu za talaka ya Kanye na aliyekuwa mkewe Kim Kardashian kukamilika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live