Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakenya wachafukwa kisa Willy Paul kununua daladala

Willy Paul Hiace Wakenya wachafukwa kisa Willy Paul kununua daladala

Mon, 26 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mitandao ya kijamii hasa kurasa za kiburudani nchini Kenya, zimechafuka kuhusiana na Msanii Willy Paul kununua gari moja aina ya Hiace na kuifanya Matatu (Daladala) na kuita press kwaajili ya ishu hiyo, na ukiwa ni uwekezaji mkubwa zaidi kwa msanii huyo tangu aanze muziki miaka kadhaa iliyo pita.

Asilimia kubwa ya comments za wakenya wanadai Muziki wa Kenya ulishakufa, na wasanii wana majina makubwa lakini pesa hawana, ni wachache sana wenye nazo zinazo tokana na sanaa wanayo fanya.

Moja ya mdau, amecomment kwenye page moja ya Udaku nchini humo, akidai maisha bado hayana balance, Wakati Diamond akinunua Ndege, Willy Paul bado yuko kwa Matatu (Daladala), Comment hiyo imefanya baadhi wajibu kuwa Diamond si wa kufananishwa na Wasanii wengine, mwingine akimcheka mtoa Comment kwa kuuliza akili za Kumfananisha Willy Paul na Diamond kazitoa wapi.

Lakini pia wapo walioona Willy Paul kafanya uwekezaji mkubwa na ipo siku mambo yatakubali zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live