Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakazi ndani ya albamu moja na Mafikizolo, Salif Keita

Mon, 1 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Rapa kutoka Tanzania, Webiro Wasira maarufu Wakazi amechaguliwa na Bodi ya Pan Africa kushiriki katika albamu itakayowashirikisha wasanii wengine wakubwa barani Afrika.

Albamu hiyo itakayotambulika kwa jina la ‘Pan Africa’ itakayotolewa Mei 25, mwaka huu itawajumuisha wasanii kama Mafikizolo, Salif Keita , Brenda Mtambo na wengineo.

“Nilitafutwa na mtu wangu wa karibu kunifahamisha kwamba kuna ‘project’ ya kutengenza albamu. Nimeshafanya kazi nyingi za kuwakutanisha wasanii tofauti kutoka nchi mbalimbali na unajua unavyofanya muziki wako wengi wanaona na kujua nani anaweza kufanya kitu kizuri, sijafanya chochote zaidi nimekuwa nikijihusisha na muziki wa Kiafrika zaidi,” amesema Wakazi.

Amesema tayari wameshaandaa wimbo ‘My Heritage’ ambao amemshirikisha Chantel ambaye kwa mara ya kwanza anafanya naye kazi.

Albamu hiyo inatengenezwa chini ya usimamizi wa Mzilikazi wa Afrika Kusini na studio za Bomba Records.



Chanzo: mwananchi.co.tz