Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakazi azidi kumwandama Mondi "Acha maneno"

Diamond Wakazi WA0003 Wakazi azidi kumwandama Mondi "Acha maneno"

Thu, 10 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tumeona hoja na majadiliano mengi kuhusu kauli ya Rais wa WCB Diamond Platnumz kwamba wakati huu tasnia ya muziki imekuwa zaidi kuliko kipindi chochote kauli ambayo imezalisha mijadala mingi.

Rapa Wakazi amekuja na hoja ya kwamba kauli hiyo haina mashiko kutokana na vigezo ambavyo amevianisha, ila kabla hataonyesha uthibitisho wakisayansi kwamba muziki umepiga hatua kwa kiasi kikubwa, ngoja tuwamwagie maua yao wasanii kama AY aka Master mmoja kati ya wasanii waliotoa network kwa wasanii wengi, Juma Nature, Alikiba, Harmonize Lady JayDee pamoja na wasanii wengine kila mmoja amefanya kazi kwa mapana yake katika kuitangaza nchi na kukuza muziki wa Tanzania.

Turudi kwenye hoja za Wakazi, ni kweli muziki unaweza kupimwa na ushamiri wa tasnia kiuchumi, miundombinu, ubora wa kazi, mfumo wa uzalishaji na uendeshaji, ila sio kweli vyote vinafanya vibaya.

UCHUMI WA TASNIA

Uchumi ambao unazungumzwa ni uchumi wa msanii binafsi pamoja na tasnia kwa ujumla. Hapa tunazungumzia jinsi sekta ya muziki ilivyokuwa na mchango katika uchumi wa nchi kuliko kipindi chochote.

Uundwaji wa Wizara ya Sanaa ni moja kati ya ishara ya ukuwaji wa sekta hii ambayo kwa sasa inachangia pato la taifa ambapo kwa bajeti 2022/23 sekta ya Sanaa inatarajia kukukusanya Tsh Bilioni 9.

Pia tasnia imezalisha na kuongeza mnyororo wa thamani katika sekta nyingine kama sekta ya ushonaji, mitindo, urembo, utalii wa ndani, kampuni za uzalishaji wa video, dansa pamoja sekta nyingine ambazo moja kwa moja zinanufaika na sekta ya sanaa.

Ukuwaji huo unaendana sambamba uanzishwaji wa mfuko wa sanaa ambao umeweza kuwakopesha mitaji wasanii zaidi ya Tsh Bilioni 1 zimetolewa kitu ambacho hakijawahi kufanyika katika miaka ya nyuma, kwa nini huu usiwe wakati bora zaidi wa sanaa?.

UCHUMI BINAFSI, DIAMOND KAMA MFANO

Kila mmoja atakubaliana na hoja kwamba huu ndio wakati umetengeneza wasanii wengi walioimarika zaidi kiuchumi.

Miaka ya nyuma wasanii ukisikia wanamiliki magari, nyumba za kifahari au muziki production basi jua ni mameneja na watu wenye pesa walikuwa wanawezesha. Miaka ya sasa mambo yamebadilika sana wasanii ndio wanaajiri mameneja, vyumba za kifahari pamoja na kufanya muziki promotion. Mfano wa wasanii kama hao ni Harmonize, Alikiba, Diamond, Kusah pamoja na wengine wengi wametoka kwenye mfumo kutegemea kila kitu na kuwa wasimamizi.

Diamond ni mmoja kati ya wasanii hao, na ni mfano wakuigwa na ndio maana amekuwa akitolewa mfano na viongozi, waandishi pamoja na majarida mbalimbali. Ukweli mchungu huo umezalisha chuki, ukiongea ukweli basi unajipendekeza, nani sasa mwingine wakutolewa mfano zaidi yake, RayVanny ambaye ameanza kufanya vyema Ulaya ni zao la Diamond, Harmonize naye ni mtoto wa Diamond nani mwingine. Alikiba aliamua siku nyingi kubaki na game la nyumbani, mkimtaja huko utakuwa unamuonea tu.

Ni kweli zamani kuna wasanii walifanya makubwa, historia imeandikwa na akiwa AY, Juma Nature, Remmy Ongora lakini katika miaka hii, nani wakumzidi Diamond kuanzia kwenye idadi ya tuzo za Kimataifa alizokuwa nominated pamoja na alizochukua, show za kimataifa alizofanya, kolabo za kimataifa alizofanya, jina lake kuwa mention na mastaa wakubwa, interview na vituo vikubwa vya runinga, yote haya yanadhihirisha mwamba amepambana na kuiweka Tanzania katika ramani ya muziki ambayo haikuwahi kutokea bila mifumo rasmi ambayo wanaubiria wengine hapa wazungu wanasema “Hard work beats talent when talent fails to work hard.”

Diamond amejihimarisha kimuziki na kibiashara katika level za P. Diddy, Jay Z kibongo bongo, ni kama maji usipomnywa utampikia tu, hakuna namna yakumkwepa kumtaja kwenye kila kona, ni mmoja kati ya wasanii ambao wanalipa kodi kubwa kupitia shughuli za sanaa kwa mujibu taarifa za Mamlaka ya Mapato Tanzania ambayo amewahi kuzibaonisha mwenyewe.

KUHUSU SHOWS NA CORPORATE ENDORSEMENTS

Tukizungumzia ukuwaji wa muziki kwa kuangalia kigezo cha shows lazima tuangalie mambo mengi.

Mosi ni kuangalia historia za show kubwa za uko nyuma zilikuwaje kulinganisha na sasa, jinsi zilivyotoa fursa na jinsi ukuwaji wa teknolojia ulivyobadili tabia nyingi za mashabiki. Hili litatufanya tukubali nyakati zimebadilika kabisa, show za matamasha ambazo zilikuwa zinatengemewa na wasanii wengi wa BongoFleva zimepotea kutokana na mabadiliko hayo, Summer Jam, Fiesta, Kill Tour, Muziki Mnene pamoja na Wasafi Festival ni moja kati ya matamasha yaliyowahi kutokea nchini Tanzania.

Tamasha la Fiesta ambalo ni moja kati ya tamasha kubwa kuwahi kutokea Tanzania limekuwa likisuasua katika miaka mitano ya mwisho, ingawa mwaka 2022 lilirudi kwa nguvu na kasi kubwa, hili tutalizungumza siku nyingine lakini bado halijaleta matokeo chanya kama zamani.

Wasafi Festival pamoja na matamasha mengine kama Muziki Mnene bado hayajatoa fursa kubwa kama Fiesta ya miaka ya nyuma, fursa hizi kwanza ni kama idadi ya wasanii wanaoshiriki, uibuaji vipaji, mnyorororo wa thamani kwa sekta mtambuka na kubwa zaidi ni idadi ya mikoa ambayo tamasha linazunguka.

Haya yote hayapatikani kwa sasa yamesababishwa na mabadiliko ya biashara hiyo yaliyochochewa na teknolojia ambayo siku nyingine tutaieleza zaidi ila kwa ufupi tu kwa sasa dunia ni kijiji, mashabiki wa sasa anaweza kuchagua anachokitaka hata kwa wasanii wa nje, yaani soko ni moja na WizKid na Burna Boy na mastaa wengine wa Afrika Magharibi kwahiyo wasanii wasipokuwa wabunifu katika kazi zao waambulia patupu kwenye biashara nzima ya muziki, hapa ni utunzi, promo pamoja na life style ya msanii, show na biashara ya muziki kwa wengi itaonekana zimeanguka na kwa wachache wajanja watapiga hela, mbaya zaidi wenzetu kama Nigeria na Afrika Kusini wana idadi kubwa ya watu kila kona ya dunia, kwa maana hiyo tumuelewe Diamond anaposema kimataifa kunahitaji kusaidaiana sio kuwavunja nguvu ambao tayari wamefanya kitu.

Wakazi ni mmoja kati ya wasanii wazuri wa hip hop, hoja zake ni nzuri kama angekuwa anafanya biashara ya muziki. Darasa kupitia Muziki Gani alisema “Acha Maneno weka muziki” ili uwe mfano kwa wasanii wengine, unachokitaka kifanyike ukifanye kwa vitendo wakati mwingine sio kila anayekupigia makofi anakuunga mkono, wana Kuchora, umalize hoja zako waendelee na ajenda zao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live