Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakazi ampa makavu Mondi "Kisingizio cha Lugha ni cha kijinga"

Wakazi Na Diamond Wakazi ampa makavu Mondi

Wed, 9 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Spanner za rapa Webiro Wakazi Wasira anaendelea kumshushia supatsaa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kama ambavyo ameahidi.

Hii ni baada ya Diamond kudai kuwa muziki wa Bongo bado upo chini hivyo akawasihi wasanii wenzake kuungana ili kuupaisha muziki wa Tanzania kama ambavyo Wanigeria na Waafrika Kusini wanafanya.

Kupitia ukrasa wake wa Instagram, Wakazi ameandika;

HII HAIJAENDA (Part Two)

Aka “Huo ni uongo”

Kisingizio cha lugha ni cha kijinga. na kisingizio cha Network pia.

West Africans wana lugha zao, na asilimia kubwa wanaongea Pigdin English ambayo ni kama kiswahili tu maana hamna mtu ulaya au marekani anakielewa. Hiyo sio advantage hata kidogo… na kusema kuhusu kwenye ramani wapo karibu, ni ujinga maana international sio US and UK only, bali hadi Australia na Japan.

Hii point ya kusema Wabongo hawafanyi Entertainment ni UONGO. Wewe mwenyewe unaletwaga huku na kina Ligate, DMK Global na Inno wa Safari Ent. Pia kuna Wasanii kibao hapa marekani tu; Erica Lulakwa, Big Stickerz, Mr TZ, Gwaii Thyword, Darda King, Ebreezy, Roma, etc.

Pia Wabongo kibao Wamejiajiri na ni wafanyabiashara, na sio hivyo unavyosema eti wanafanya kazi rasmi tu.

HAWAJI KWENYE SHOW SABABU HAUJAWAPA SABABU YA KUJA! Unafanya show kimazoea badala ya kuwaonyesha watu thamani. Hau engage na community, hauonyeshi growth ya performance, mnadhani vioja vya Instagram vinatosha kufanya muweke ridiculous prices ambazo ukiangalia na kinachofanyika haviendani.

Na nikujuze tu, show za Wa west wanajaza sio tu wao, bali hadi wanyamwezi! They push and then they show value!

Network ni mtandao! sio kiingereza. MTANDAO HUJENGWA. Jux na Bdozen, Rich Mitindo wana network China AY anayo SA, Kenya, US, Naija…

USIPOTOSHE WA TZ, SISI TUPO KWA GROUND, TUNAJUA UKWELI. Badala ya kuleta visingizio, ni muhimu kujitathmini na ku-restrategize… Hata sisi tukishindwa kuwika hapo home, tunarudigi kwenye drawing boards.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live