Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakazi amlipua tena Diamond "Sio kweli, unadanganya"

Diamond Wakazi WA0003 Wakazi amlipua tena Diamond

Wed, 9 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Spanner za rapa Webiro Wakazi Wasira anaendelea kumshushia supatsaa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kama ambavyo ameahidi.

Hii ni baada ya Diamond kudai kuwa muziki wa Bongo bado upo chini hivyo akawasihi wasanii wenzake kuungana ili kuupaisha muziki wa Tanzania kama ambavyo Wanigeria na Waafrika Kusini wanafanya.

Kupitia ukrasa wake wa Instagram, Wakazi ameandika;

HII HAIJAENDA! (Part One)

Kwanza sio kweli kuwa sasa hivi muziki wetu ndio umeinuka. Infact kuinuka kwa muziki kunapimwa na ushamiri wa tasnia kiuchumi, miundo mbinu, ubora wa kazi, mfumo wa uzalishaji na uendeshaji, nk.

Karibia vyote hivyo vinafanya vibaya, kinachoonekana ni ushindani tu kati ya baadhi ya Wasanii.

• Wasanii hawapati shows

• Hamna Corporate Endorsements

• Miundo Mbinu bado mibovu

• Mnyororo wa Uzalishaji bado haunufaishi (Msanii tu ndio walau, ila Producer, mpiga Bendi, dancer, meneja, DJ, Video vixens, songwriters, etc bado)

• Quality ya muziki bado inasuasua (hapo hatujagusia lack of Identity)

SO HIYO KAULI YAKO SIO SAHIHI!

Pili, yea sisi kimuziki bado… nakubali ila je ni bado kulingana na nani, na bado kwenye sekta ipi?! Maana Africa ina nchi kama 54, sasa tukizidiwa na 7 isiwe ndio kusema bado.

Tanzania kuna vitu tunavyo na tunavipatia, na huko zamani ndio tulivipatia kabisa… sema kwenye ulimwengu wa kisasa na muziki wa “duniani” ndio tunafeli.

Walau zamani tulikuwa na Wasanii wanafanya poa kimataifa, kulikuwa na diversity, kulikuwa na ka Uchumi hauweni.

• Remi Ongalla yupo hadi kwenye soundtrack ya Hollywood (“Kipenda Roho” on Natural Born Killers)

• Rappers wa TZ (Sugu, Xplastaz, AY, Prof Jay) walipata mashavu international

• Msanii zaidi ya mmoja aliheshimiwa kwa Tuzo za nje (Jide, AY, Tid, Prof Jay, Fid Q, Sir Nature)

• Tuzo washindi walipata hela, zilizaa tours, wakapata hela tena

• Wasanii waliweza andaa sho zao zikalipa.

• Tuliweza kuzalisha new stars, sasa hivi ni kama tumegoma au tumeshindwa.

SO HOJA YAKO HAIJAENDA. Na kuhusu kukatisha Tamaa, Hamna aayefanya hivyo labda wewe ambae una support only wale ambao unanufaika nao kiuchumi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live