Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakazi: Singeli Unachukua ya Hip Hop Bongo

WAKAZI Wakazi

Wed, 21 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rapa maarufu Bongo, @wakazi ameibuka na kudai kuwa muziki mpya wa singeli unakuja kwa kasi kuchukua nafasi ya HipHop nchini.

Wakazi amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya kupost ngoma mpya ya dullamakabila;

''THIS IS NICE @dullamakabila ????????

Maudhui ✅ Ubunifu wa wimbo ✅ Ubunifu wa video ✅

Sound ya Singeli ni unorthodox, ikimaanisha ni ya kipekee na kitofauti, hivyo inaeleweka kama kuna watu hawatoipenda au ku-relate nayo. Ila mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni. Singeli imepiga hatua kubwa na inafurahisha kuona umekuwa ni commercial mainstream music sasa (social platform trending) ????????

Wiki kadhaa zilizopita nilizungumza kwenye kongamano la ACCES (clip ipo inazunguka shot by wasafi media) na nilisema kuwa nina amini kuwa Singeli imechukua au inaenda kuchukua nafasi ya Hip Hop, kama muziki wa uhalisia wa maisha ya kila siku, na wenye maudhui ya kufikirisha. YAANI KIUFUPI THEY KEEP IT REAL.

Meja Kunta, Sholo Mwamba,Kinata Mc na hadi Dula Makabila (na wana kibao tu wengine), wanaibeba bendera vizuri. Na it is a nice thing kuona inapokelewa kwa ukubwa. HONGER DULLA, KAZI NZURI

ILA HONGERA KWA WOTE WANAOIFANYA, INUA NA KUIPIGANIA SINGELI.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live