Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Wajawazito wanaokunywa pombe kushtakiwa

Wajawazito Wanaokunywa Pombe Kushtakiwa Wajawazito wanaokunywa pombe kushtakiwa

Thu, 7 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Akizungumza katika kongamano la kukuza uelewa kuhusu athari za unywaji pombe kwa wajawazito nchini Afrika Kusini, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Hendrietta Bogopane-Zulu amesema unywaji wa pombe husababisha madhara kwenye ubongo wa watoto.

Hivyo amesema akinamama wanaokunywa pombe wakati wa ujauzito nchini humo washitakiwe maana ni unyayasaji wa watoto.

Kwa mujibu wa takwimu, matumizi ya pombe nchini humo imeripotiwa kufikia 41.5% kwa wanaume na 17.1% kwa wanawake, wakazi wa mijini ni 33.4% na wa vijijini 18.3% hali hiyo imeonekana kuwa tishio kwa taifa hilo watu kuzidi kuathirika na ulevi wa pombe.

Aidha, Hendrietta ameeleza Shirika la Afya Duniani WHO limeitaja Afrika Kusini kuwa na kiwango cha juu zaidi cha walevi wa pombe duniani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live