Zaidi ya waigizaji na watu mashuhuri 120 kutoka China wamewasili Zanzibar kwa ajili ya kuanza kutengeneza filamu maalum ya uhusiano wa nchi hiyo na Bara la Afrika katika sekta ya Afya.
Ugeni huo ambao umewasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume leo majira ya saa 12 asubuhi na ndege ya Air Tanzania wakitokea china umepokelewa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Waziri wa Afya Zanzibar Mheshimiwa Nassor Ahmed Mazrui ambapo ametaja dhumuni la ujio wao ni kwa ajili ya kutengeneza filamu ya Afya iliyopewa jina la "milele" ikiwa ni hatua ya kuthamani mashirikiano kati ya Chini nan chi za Afrika ikiwemo Tanzania
Afisa kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini China Miraj Ukuti Ussi amesema mbali na uandaaji wa filamu hiyo kwenye sekta ya afya pia itatoa msukumo wa kuvitangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini katika anga za kimataifa.