Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wahuni wamharibia Khaligraph Jones kwa Rick Ross

Khaligraph Jones Rick Ross.png Wahuni wamharibia Khaligraph Jones kwa Rick Ross

Thu, 21 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rapa Khaligraph Jones amefunguka chuki ya wazi aliyofanyiwa na wakuda baada ya kushindwa kwenda 'Instagram Live' kuzungumza na The Biggest Boss Rick Ross.

Khaligraph Jones ametoa malalamiko hayo akisema; "Leo ndio nimeshuduia kiwango kikubwa cha chuki dhidi yangu".

"Nilitakiwa kuwa na Live na Rick Ross lakini haijatokea hivyo sababu inaonekana baadhi ya watu wanaoenda kinyume na mimi wameiripoti akaunti yangu nimeshindwa kupata access ya kwenda live".

Khaligraph amemaliza kwa kuomba radhi mashabiki zake waliokuwa wanasubiri mazungumzo yake na Rozay na ratiba ya kupiga naye story imepangwa upya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live