Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wahuni sio watu wazuri! Binti wa kazi wa Harmonize apachikwa mimba

HARMONIZE SDF Harmonize na Chef

Fri, 28 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Moja ya headlines zinazokimbia kwa sasa ni kuhusu dada wa kazi wa supastaa wa Bongo Fleva, Harmonize aitwaye Chef Rehema kupata ujauzito.

harmonize amefichua habari za ujauzito wa Rehema jana Alhamisi kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo alipakia video ikionyesha tumbo lililochomoza la mpishi huyo wake.

Katika video hiyo, Harmonize anasikika akimwita mpishi huyo wake kuja mahali alipokuwa ametulia na kamera yake. Punde baada ya Rehema kujitokeza mbele ya Camera, bosi huyo wake anasikika akimpongeza.

"Mbona unajificha Chef Rehema?" Harmonize alimuuliza Rehema kabla ya kutokea.

Baada ya Rehema kujitokeza, bosi huyo wa Kondegang kwa sauti kubwa anasema "Hongera! Chef Rehema Hongera!"

Katika maelezo ya video, mwimbaji huyo anashangaa jinsi mjakazi huyo wake alivyopachikwa ujauzito.

"Wanaume hawachezi OOO!! Lol, tayari wamefanya yao kwa dada wangu wa kazi. Sasa wamepenyaje KONDE VILLAGE?? Jamani wahuni sio watu," aliandika.

Alimpongeza mwanadada huyo kwa ujauzito na kueleza hamu yake kubwa ya kukutana na mtoto anayebeba tumboni.

"Hongera Rehema, Uncle Konde ako hapa akisubiri mwanachama mwingine wa Kondegang," alisema.

Sio mengi yanayojulikana kumhusu mjakazi wa Harmonize, Chef Rehema na anaonekana kuwa mwanamke mwenye haya.

Takriban miezi mitano iliyopita staa huyo wa Bongo alitoa ahadi ya nyumba na gari kwa mjakazi wake mwingine, Zuwena.

Alichukua hatua hiyo kama ishara ya shukran kwa huduma alizomtolea katika kipindi cha miaka saba ambacho kimepita.

Wakati huo, Konde Boy alitangaza kuwa anapanga kutimiza hadi yake kwa Zuwena kabla ya mwezi huo kuisha.

"Ni kama shangazi yangu. Miaka 7 anajua nakula nini. Ananipikia, ananifulia, ananifanyia usafi, anajua ukichaa wangu wote. Kabla ya Juni namnunulia gari lake la kwanza na kinyumba hata cha chumba 3 mkoani kwao," alitangaza.

Harmonize alifichua kuwa Zuwena ndiye mjakazi wake wa kwanza huku akidai kuwa sio mfanyikazi wake tu bali pia ni kama dada yake.

Alimshukuru sana mwanadada huyo kwa kazi kubwa ambayo amekuwa akifanya na kumtakia baraka za Maulana.

"Mungu akubariki dada Zuuh maana si kwa vipipi vya sigara ambavyo unavifagia kila siku kwenye mashuka majivu vipi," Alisema.

Harmonize anajulikana kuwatambua na kuwazawadi watu wake wa karibu baada ya kupiga hatua muhimu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live