Kuvumbua kitu cha kipekee na kuleta mabadiliko katika historia ya mwanadamu ni jambo ambalo linaleta hisia za kufurahisha na kuridhisha nafsi ya mbunifu.
Ni jambo jema na la kufurahia kwa wale ambao walikuwa nyuma ya ubunifu mzuri wa mambo mbalimbali kama gurudumu, saruji, injini au mtandao.
Hata hivyo, si ugunduzi ama uvumbuzi wote unaleta manufaa ulimwenguni; wapo ambao kusema ukweli wameacha ugunduzi kusikitisha na wa kutisha ulimwenguni.
Kalashnikov 'alihofia na kujilaumu kwa mauaji ya bunduki aliyovumbua ya AK-47 Kuna tofauti gani kati ya bunduki ya AK 47 na M16? Na baadhi ya wawagunduzi hawa wameishia kuteswa na dhamiri zao.
Hawa ni wagunduzi wanne kati yao ambao, mara nyingi bila kupima nguvu za uharibifu za ubunifu wao, waliishia kuleta baadhi ya silaha mbaya zaidi katika historia ya dunia.
1. Robert Oppenheimer, "baba wa bomu la atomiki":
Hakukuwa na mwanasayansi mwingine aliyehusishwa kwa karibu zaidi na ugunduzi na utengenezaji wa mabomu ya atomiki wakati wa Vita Kuu ya pili ya dunia kuliko Robert Oppenheimer.
Mwanafizikia wa kinadharia wa Marekani alikuwa mkurugenzi wa Mradi wa Manhattan, ambao uliweza kutengeneza bomu la kwanza la atomiki katika historia ya dunia.
Bomu hilo likatumika kulipuliwa katika jangwa la New Mexico - katika operesheni iliyoitwa "Utatu" - mnamo Julai 16, 1945, chini ya mwezi mmoja kabla ya kurushwa kwa mabomu huko Hiroshima na Nagasaki, nchini Japan, ambapo inakadiriwa kuwa watu kati ya 150,000 na 250,000 walipoteza maisha.
2. Arthur Galston na Kemikali iliyoitwa 'Agent Orange'
Mwanabiolojia wa mimea wa Marekani na mwanafiziolojia Arthur Galston hakuwahi kufikiria kuwa alikuwa akiunda kitu ambacho kinaweza kutumika kama silaha: kitu kinachoitwa Agent Orange.
Eneo lake la utafiti lililenga homoni za mimea na athari za mwanga kwenye ukuaji wa mimea, lakini ugunduzi wake ukaibua silaha hiyo, iliyotumika na Marekani katika vta vya Vietnam kati ya mwaka 1962 na 1971.
Kemikakali hii ya 'Agent Orange', ilitumika na jeshi la Marekani kupulizia kwneye miti, na vichaka wanakoweza kujificha wanajeshi wa Vietnam.
Inasadia kunyausha na kudondosha majani yote kwenye miti kwa muda mfupi na kuwafanya maadui (wavietnman) kuonekana kirahisi na jeshi la Marekani
Kwa hivyo, kuanzia mwaka 962 hadi 1970, wanajeshi wa Marekani walitengeneza takriban galoni milioni 20 za dawa hiyo ili kuharibu mazao na kufichua maficho na njia za maadui zao.
Mbali na kemlikali hiyo kupigwa marufuku baadae, Mgunduzi mwenyewe alidai kuwa "sayansi ilitumika vibaya."
"Sayansi inalenga kuboresha hali ya ubinadamu, sio kuipunguza au kuharib, na matumizi yake kama silaha ya kijeshi yalionekana kutofaa kwangu," aliongeza.
3. Mikhail Kalashnikov, mgunduzi wa bunduki ya AK-47:
Ni mbunifu wa moja ya silaha zinazotambulika zaidi duniani: bunduki ya nusu-otomatiki ya AK-47.
Mnamo 1947, Mikhail Kalashnikov wa Urusi aliunda bunduki hii rahisi, sugu na ya kuaminika ambayo ikawa silaha muhimu kwa majeshi ya Soviet na Urusi, pamoja na nchi zingine kadhaa.
Pamoja na ugunduzi huo, katika maisha yake yote Mikhail Kalashnikov alionyesha majuto kiasi kwa uvumbuzi wake mbaya - "Nalala fofofo," aliwahi kusema - alikiri muda mfupi kabla ya kifo chake kwamba alikuwa katika "maumivu makali ya kiroho."
4. Alfred Nobel na baruti:
Akizaliwa katika familia ya wahandisi, Nobel alifanya kazi na baba yake katika utengenezaji wa vilipuzi. Lakini mnamo 1864 alikutana na tukio la kutisha ambalo liligusa maisha yake, wakati mdogo wake wa kiume na watu wengine wanne waliuawa katika mlipuko wa nitroglycerin.
Miaka miwili baadaye, mwaka wa 1866, Nobel alibuni mbinu iliyoruhusu kilipuzi kisicho imara kushughulikiwa kwa usalama. Ili kupunguza hatari, alichanganya 'nitroglycerini' na nyenzo ya kufyonza ya vinyweleo, hivyo kutengeneza baruti.
Uvumbuzi huu ulimpatia utajiri mkubwa na umaarufu.. lakini pia ulileta uharibifu. Naam, haikuchukua muda mrefu uvumbuzi wake kuanza kutumika kwa madhumuni ya kijeshi.
Walitumia katika makombora mbalimbali na risasi na kusababisha mamia ya maelfu ya vifo.
Bila shaka Nobel aliyekufa mnamo Desemba 10, 1896 nyumbani kwake San Remo, Italia, alijutia ugunduzi wake huo.