Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wagosi waliingia Dar kama barua yenye stamp na care of

Bao Full Wagosi Wagosi waliingia Dar kama barua yenye stamp na care of

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Miaka 22 iliyopita, Wagosi wa Kaya, walisafiri kutoka Tanga hadi Dar es Salaam, mithili ya barua yenye stamp na care of.

Profesa Jay ndiye mwezesha safari. Akawagonga stamp Tanga. Akawaambia, mkifika Ubungo, ongozeni mpaka Sinza Mori. Care of ni Profesa Ludigo. MJ Production, Masaki, ndio main address.

Usafiri wa kufika Dar kutoka Tanga ni hisani ya rafiki wa kila mtu, Fredy Tayasar. Mfukoni walikuwa na Sh50,000, walizopewa na Rogers Mynas kwa ajili ya kulipia studio.

Mwonekano wao tofauti na utamaduni wa walichojinasibu kukifanya. Suruali za vitambaa na mashati ya bahama. Chini four angle shoes. Havioani na personalities za Hip Hop.

Ludigo ni Mnyamwezi minded. Alisimama getini na kikombe cha chai. Akawaambia Wagosi “simameni hapohapo”. Akawatazama juu mpaka chini. Akauliza: “Ninyi mnajua kurap kweli?”

Balaa lilikuja Ludigo alipowaambia wamchanie mistari palepale getini, nyumbani kwake. Wagosi walifungua Mzinga wa Nyuki. Tanga Kunani haikufika kati, Ludigo alitelekeza kikombe cha chai getini, akawaambia Wagosi; “Twendeni.”

Safari kutoka Sinza hadi Masaki MJ. Moja kwa moja studio. Pishi Tanga Kunani likaiva. CEO wa MJ, Master Jay, aliposikiliza pini, akasema “sichukui hela yenu”. Kisha, aliwaalika major players wote wa Bongo Flava League kusikiliza divine kutoka Tanga.

Wimbo Tanga Kunani uligombewa studio. Kila mtu aliuchota ili akawe wa kwanza kuucheza redioni. Maulid Kitenge alishinda battle alipovunja sheria, akaucheza Tanga Kunani kwenye kipindi cha michezo, Spoti Leo, Radio One. Ni mwaka 2001.

Ile safari ina neema nyingi. Wagosi wa Kaya ni kurunzi lililomulika kila kero ya kijamii Tanzania. Usiongee “Wauguzi”, “Traffic” wala “Taxi Driver”, Wagosi walimlazimisha hadi “Kibaka” kuokoka.

Utumishi wao uliotukuka ndio sababu Bongo Flava Honors watawatunuku Wagosi wa Kaya plaque maalum, kutambua mchango wao wenye thamani kubwa kwenye ukuaji wa Bongo Flava na sanaa Tanzania.

Shughuli ni Oktoba 27, 2023. Alliance Francaise, Upanga. Siku hiyo, Wagosi watapiga shoo ya live band nyimbo zao zote.

Mwenyeji wa shughuli ni The Godfather, Sugu The Jongwe.

Ndimi Luqman MALOTO

Chanzo: www.tanzaniaweb.live