Jitihada za kuipeleka Swahili Rap mjini, zilikunisha vichwa magwiji. Ubunifu ulileta mitindo anuwai. Huu muziki uliingizwa mainstream kwa gia kubwa.
Project ya Uchagani “Raphael” ya tall wa Kisukuma, Freddie Saganda, ilibadili masikio ya wengi. Michano ya Kiswahili chenye lafudhi ya kilugha, ulevi, wapo waliorap wakiwa usingizini.
Seleka la Tanga lilitua Dar es Salaam, MJ Production. Mtu bee na rapping za lafudhi za kilugha, Kidigo na Kisambaa. Waliyavaa matatizo ya kijamii kwa hisia na kuyapazia sauti kama Musa na Torati.
Charity begins at home; “Tanga Kunani” off the charts. Mdigo na Msambaa, waliifanya agenda ya mkoa wao kuwa kesi ya kitaifa. “Tanga kunani palee, mbona kila kitu kimekwisha.” Taifa zima liliimba.
Mdigo ni Dr John. Msambaa ni Mkoloni. Gang ni Wagosi wa Kaya. Moto uliwaka walipodeal na unoko maofisini. Wakamleta John Woka kwenye ramani, chupuchupu atapikie mic akiwa bwax. Wimbo “Vinatia Uchungu”.
My God, Wagosi waliuzungumza ujumbe wa kila Mtanzania katika “Wauguzi”. Madaktari na manesi walichezea jabs za kutosha ndani ya beti tatu za Wagosi.
“Titamtambuaje” ni muziki mawaidha. Ngumu mno kutambua mahali wadudu wa HIV walipoweka maskani. Usipime kwa macho mtu wangu.
Sauti za Wagosi zilikuwa juu mno walipoimba “Kero”. Again, Wagosi waliimba ujumbe wa kila Mtanzania kuhusu umeme na maji. “Soka la Bongo” hawakuliacha. Halafu ile “Nyeti” brothers and sisters.
Kila msafiri aliimbiwa katika “Safari Zetu”. Waungwana wa barabarani walikula za chembe kwenye “Traffic”. Kutoka “Ukweli Mtupu” hadi “Ripoti Kamili”, Wagosi waliigonga serikali, wakaitikisa mitaa. Waliuzungumza ukweli unavyopaswa kuzungumzwa.
Wagosi ni tafsiri ya social justice musicians. Wanamuziki wanaopigania usawa wa haki za kijamii. Serikali na mikataba mibovu waliimba “Tumeshituka”. Halafu “Bao” ni comic with message.
Oktoba 27, 2023, Wagosi watatunukiwa hadhi maalum ya Bongo Flava Honors, kwa mafanikio ya muziki wao. Ni siku ya kuwaheshimisha machampioni wa social justice Tanzania.
Burudani ya nyimbo zote za Wagosi kwa live band jukwaani. Sherehe kamili ni Alliance Francaise, Upanga.
Ndimi Luqman MALOTO