Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafahamu wazazi wa Burna Boy

Burna Boyss Wafahamu wazazi wa Burna Boy

Mon, 4 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mama wa supastaa wa Muziki Afrika, Damini Ebunoluwa Ogulu 'Burna Boy', Bi. Bose Ogulu ndiye meneja wa kazi za muziki za mwanae, ajitosa kusherehekea miaka 33 ya ndoa yake na baba Burna Boy aitwaye Samuel Ogulu.

Yeye na mume wake huyo walifunga ndoa mwaka 1990 na wamejaaliwa watoto watatu ambao ni Burna Boy(32) na wadogo zake wenye miaka 30 na 29.

Mama mzazi wa Burna Boy ni msomi wa degrees za vyuo vikuu hasa katika lugha za kigeni na tafsiri za lugha, anazungumza vizuri lugha 6 ambazo ni kiingereza, kifaransa, kiitaliano, Kijerumani na Kiyoruba na Pijini english ya Nigeria.

Kwa miaka kumi alifundisha Kifaransa katika chuo kikuu cha elimu Hartcourt, Nigeria pia aliwahi kuwa mtafsiri lugha katika Federation of West African Chambers of Commerce.

Aliamua kuacha kazi huko kwingine na kuamua kujikita zaidi kiwanda cha muziki alikoona kuna maslahi zaidi hasa kumsimamia mwanae ambapo Burna Boy mwenyewe ndie alimuomba mama yake awe meneja wake baada ya kuona ana uwezo mkubwa katika hilo.

Mwaka 2021 Bilboard ya Marekani katika orodha yao ya Internationa Powers Players List kutambua mchango wake kwa anachokifanya katika ulimwengu muziki ambapo mwanae kwasasa sio tu superstar mwenye mafanikio katika muzika bali ameweza kukubalika hata kidunia ikiwemo Amerika na Ulaya.

Baba wa Burna, Mzee Samuel alizaliwa Februari 4, mwaka 19960 huko Mbiama Nigeria, yeye ni mfanyabiashara na mmiliki kiwanda cha kuchomelea vyuma 'welding'.

Wazazi wa Burna Boy wameonekana wakisherehekea Universary ya miaka 33 ya ndoa yao nchini Nigeria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live