Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wadudu sio wahalifu - RPC Masejo

Wadudu Chuga Wadudu OG.

Thu, 18 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema linao wajibu wakisheria wa kuwalinda raia na mali zao huku likibainisha kuwa limepokea maelekezo ya Mwenyekiti wa Ulinzi Mheshimiwa Paul Makonda aliyoyatoa hivi karibuni.

Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha SACP Justine Masejo kufuatia maagizo ya Mkuu wa Mkoa huo ambapo alilitaka Jeshi la Polisi Mkoani humo kuimarisha ulinzi na usalama ili kuwezesha biashara na shughuli nyingine za utalii kufanyika kwa ndani ya saa 24.

Akiwazungumzia vijana maarufu jijini Arusha, Wadudu OG, Kamanda Masejo amesema kuwa vijana hao siyo wahalifu bali ni kionjo cha Jiji la Arusha.

“Hawa wanaojiita Wadudu ni vijana ambao ukiwatazama ni kama wasanii kwa maana wanafanya sanaa, wanapeleka ujumbe. Kwa hiyo ukiwatazama kwa jicho tofauti unaweza kuwaelewa tofauti lakini siyo hivyo.

“Kama mkuu wetu wa mkoa alivyozungumza (Makonda) alisema kuwa ni wewe tu unavyoweza kuwatumia. Wale vijana kimsingi ni wasanii, mimi nawachukulia kama moja ya vionjo vya Arusha na siyo wahalifu.

“Kuna kundi ambalo wao wanajiita Wadudu Orijino, uhalisia wao utakuta wanavaa viatu vikubwa, suruali kubwa, wanapeleka ujumbe wao. Sio kundi la uhalifu.

"Lakini wengine wanapenda kuendesha pikipiki kwa kasi na madoido, ambayo Rc amesema hii ni sanaa pia, kwa hiyo si kama watu wanavyotafsiri,” amesema Kamanda Masejo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live