Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wabunge waombwa kuchangia Miss Dodoma

WhatsApp Image 2021 05 10 At 14.08.58.jpeg Wabunge waombwa kuchangia Miss Dodoma

Mon, 10 May 2021 Chanzo: mtanzania.co.tz

Mlezi wa Mashindano hayo ya miss Morogoro na Dodoma ambaye pia ni Mbunge wa viti Maalumu Mkoa wa Morogoro amesema kuwa jamii itambue Tasnia ya Urembo na Mitindo imekuwa chachu katika kujengewa mabinti uwezo wa kijasiriamali,kijamii na kiutamaduni.

Hayo yamebainishwa leo jijini Hapa na Mbunge huyo wakati akizindua mashindano ya Miss Dodoma yanayotarajiwa kufanyika Tarehe 21 mwezi wa 6 mwaka huu jijini Hapa.

Aidha,Mh Norah Mzeru amewaomba viongozi mbalimbali na Taasisi Binafsi na za kiserikali hususani wabunge na wafanyabiashara kuwasaidia mabinti katika tasnia ya urembo na mitindo kuwapatia michango mbalimbali ili kuweza kuendeleza Tasnia ya urembo Nchini.

“Nikiwa kama mbunge wa viti maalumu mkoa wa morogoro katika Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania nawaomba wabunge wenzangu kuchangia Tasnii ya urembo na Mitindo kwani inatoa Ajira kwa mabinti zetu pamoja na kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji nchini”Amesema Mh Norah Mzeru.

Kwa upande wake mkurugenzi wa NIKALEX LTD Alexander Nikitas ambae pia ni mwandaaji wa mashindano haya amesema kuwa hii ni fursa kwa mabinti wa mkoa wa dodoma kujitokeza kwa wingi ili kushiriki mashindano haya ambayo yatawapa nafasi za kushiriki Miss Tanzania ambapo mshindi wa kwanza mpaka wa tatu ndiye atakayepata nafasi ya kushiriki Miss Tanzania.

“Mashindano haya yanayotarajia kufanyika Tarehe 21 mwezi wa 6 mwaka huu yatahusisha wilaya zote saba za Dodoma hivyo mabinti wote mnakaribishwa kushiriki mashindano haya”amesema Alexander Nikitas

Pia Alexander Nikitas amesema jamii itambue kuwa tasnia ya urembo na mitindo imekuwa chachu katika kuwajengea mabinti kuwa wana jamii wenye kutegemewa wawapo katika mashindano haya.

Chanzo: mtanzania.co.tz