Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wabongo wampongeza Zari kwa maamuzi yake ya kuachana na Diamond

Thu, 22 Feb 2018 Chanzo: bongo5.com

Baada ya Zari kutangaza rasmi kuwa kwa sasa hayupo tena kwenye mahusiano na mzazi mwenzie, Diamond Platnumz imeonekana hatua hiyo kupokelewa kwa mtazamo chanya na baadhi ya mashabiki wa Diamond Platnumz hususani wanawake.

Picha inayohusiana

Diamond Platnumz na Zari

Watu wengi ambao walikuwa wanawafuatilia wawili hao wameonekana wakitoa maoni ya kumpongeza kwa maamuzi aliyoyachukua ya kumuacha Diamond Platnumz.

Baadhi ya maoni ambayo yametolewa kwenye posti ya Zari kwenye mtandao wa Instagram, yamempongeza Zari kwa kumwambia kuwa yeye ni mwanamke jasiri na anayejitambua.

Chanzo: bongo5.com