Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waanza kushirikiana  kunyanyua sanaa, ajira 

Fe76ac4c40271dcc8d6ebce2511de2ba.jpeg Waanza kushirikiana  kunyanyua sanaa, ajira 

Thu, 3 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

TAASISI ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) imeingia makubaliano ya ushirikiano katika kuendesha mafunzo ya kozi za sanaa na Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA) ili kuongeza ushindani katika soko la ajira.

Makubaliano hayo yalisainiwa jana na viongozi wa taasisi hizo ambao ni Kaimu Mkuu wa TaSUBa, Gabriel Kiiza na Mkuu wa TCTA, Joe Matani.

Wamekubaliana kwamba TaSUBa kwa kushirikiana na TCTA ambacho ni chuo cha Magereza, wataandaa na kutoa mafunzo ya kozi za sanaa katika maeneo ya muziki, uigizaji na ngoma kwa mafunzo yatakayotolewa kwa kipindi cha muda mfupi kwa kipindi kisichopungua mwezi moja na kisichozidi miezi mitatu kwa kila udahili.

Aidha mafunzo yatatolewa na kuendeshwa katika madarasa ya TCTA ambapo maktaba pamoja na vifaa vya kujifunzia vitakuwa vya TCTA lakini endapo TCTA itakuwa na uhaba wa vifaa vya mafunzo, vitaazimwa kutoka TaSUBa.

Vile vile, bila kuathiri Ibara ya 3(a) ya Makubaliano hayo, TCTA itakuwa na wajibu wa kuwasafirisha wanafunzi na kuwapeleka TaSUBa kabla ya kuhitimu mafunzo angalau mara moja kwa kila udahili ili kuweza kujifunza mazingira ya TaSUBa.

Awali kabla ya utiaji saini wa makubaliano hayo, Mkuu wa Chuo cha TCTA, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Matani alisema, utiaji saini wa makubaliano hayo umekuja baada ya maandalizi la muda mrefu hivyo anafarijika kwa kuwa suala hilo limekamilika na sasa kazi inaendelea.

Aliema ushirikiano huo ni fursa nzuri ya kupeana uzoefu katika mafunzo ya Sanaa na Utamaduni kwa kuwa TaSUBa ni wabobezi katika eneo la mafunzo na yatachangia kuongeza ushindani mzuri katika soko la ajira nchini.

Awali TCTA kilikuwa kikitoa mafunzo kwa askari tu lakini sasa wamepanua wigo wa mafunzo hayo kuhusisha pia raia.

Katika utiaji saini huo, Kaimu Mkuu wa TaSUBa, Kiiza alisema, tasnia ya Sanaa na Utamaduni inahitaji ubunifu ili kuiboresha na kuleta vitu vipya kila wakati kwani mbali na burudani sasa ni eneo muhimu la ajira rasmi kwa kundi kubwa la vijana ambao ni nguvu kazi katika uchumi endelevu.

Chanzo: www.habarileo.co.tz