Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WCB wapigwa chini Tuzo za Tanzania Music Awards

Wcb Tuzo Wasanii wa WCB

Sun, 20 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WASANII wa lebo ya WCB Wasafi hawakupendekeza majina yao wa nyimbo zao kuingia katika kinyang’anyiro cha tuza za Muziki Tanzania zinazoandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

Kaimu Katibu Mtendaji wa Basata, Matiko Mniko amesema, Basata iliomba wasanii kote nchini kupendekeza majina yao na vipengele wanavyopenda kushindanishwa ambapo wasanii 1,360 isipokuwa kundi la WCB Wasafi walijitokeza.

Kiongozi wa Wasafi, Diamond Platnumz hajasema chochote kuhusu sababu zilizopelekea wasanii walio katika lebo yake kutoshiriki Tuzo hizo. Hii inakua mara ya pili kwa mwaka huu WCB hawaonekani katika shughuli zinazoandaliwa na taasisi zinazosimamia sanaa nchini. Shughuli ya kwanza ikiwa ni Mirahaba iliyotolewa na Taasisi ya Hakimiliki nchini (COSOTA).

Katika Orodha iliyotangazwa usiku wa kuamkia leo Machi 20, Diamond Platnumz, Queen Darleen, Zuchu, Rayvanny, Mbosso, Lava Lava wote hawajaonekana katika kipengele chochote na hivyo kuibua mjadala miongoni mwa mashabiki na wapenzi wa muziki.

Mniko amefafanua kuwa baada ya wao (Basata) kupata majina ya wasanii, waliitisha jopo la majaji 100 ambao walipitia kazi zote zilizopendekezwa na kupendekeza wasanii wa kushindanishwa kwa kila kipengele.

“Lengo letu ilikuwa ni kufanya utoaji wa tuzo hizi uwe huru kwa wasanii wenyewe kujipendekeza,” alisema Mniko.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live