Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WCB wakiri Rich Mavoko amewashtaki

11864 Pic+mavoko TanzaniaWeb

Tue, 14 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Uongozi wa lebo ya WCB inayoongozwa na mwanamuziki Diamond Platnumz, umekiri kuitwa Baraza la Taifa la Sanaa (Basata), baada ya kuwepo sintofahamu baina yao na Rich Mavoko ambaye ni mmoja wa wasanii wanaowasimamia.

Hayo yamebainika leo Agosti 14 ikiwa ni siku chache tangu Basata kueleza kuwa imepokea malalamiko kutoka kwa Mavoko kuhusu kutoridhika na mkataba alioingia na WCB.

Akizungumzia hilo mmoja wa meneja wa Diamond, Sallam Sharraf, amesema ni kweli wamepata wito wa Basata na sasa wapo katika mazungumzo.

Sallam ambaye hakuwa tayari kuliongelea suala hilo kiundani, amesema ni vyema watu wakasubiria yatakayoamuliwa huko, ambapo wanaamini Basata itauambia umma nini kilichoafikiwa badala ya wao  kuwa wasemaji.

Katika hatua nyingine Diamond amemkabidhi zawadi ya gari mshindi wa Diamond Karanga, gari aina ya Ractis aliyoshinda katika bahati nasibu iliyoanza Machi mwaka huu.

Mshindi huyo Bakari Saidi ambaye ni muuza mitumba maeneo ya Ubungo, amesema hakutegemea kushinda gari hilo na kushukuru wasafi kuja na shindano hilo ambalo amedai limebadilisha maisha yake.

Chanzo: mwananchi.co.tz