Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WCB wafunguka ishu ya Diamond kupigwa chupa

Diamond+pic WCB wafunguka ishu ya Diamond kupigwa chupa

Tue, 3 Nov 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By NASRA ABDALLAHKama ni mfuatiliaji katika mitandao ya kijamii, moja ya habari iliyoteka mitandao hiyo jana na leo ni sakata la msanii Diamond Platnumz kurushiwa chupa akiwa kwenye shoo nchini Malawi.

Diamond amekuwa nchini humo mwishoni mwa juma lililopita kwa ajili ya show ambayo alikuwa aifanye siku ya Jumamosi.

Hata hivyo siku hiyo ilipofika alishindwa kutumbuiza na kutupia taarifa katika ukurasa wake wa Instagram kuwa sababu za kushindwa kufanya hivyo ni kutokana na kunyesha mvua kubwa.

Jana Novemba 2, 2020 kulisambaa video kwenye mitandao ya kijamii ikiwaonyesha mashabiki wakiwa wanarusha chupa katika jukwaa ambalo Diamond alipaswa kupanda na kuzua maswali mengi kuwa ilikuwaje wakafikia hatua hiyo.

Mwanaspoti limeutafuta uongozi wa WCB na kufanikiwa kuzungumza na mmoja wa mameneja wa lebo hiyo, Sallam Shariff.

Akielezea mkasa mzima, Sallam amesema katika shoo aliyokwenda Diamond, lilikuwa ni tamasha la siku tatu lililoanza tangu siku ya Ijumaa Novemba 30.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz