Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WAANDISHI 8 TSN WATEULIWA KUWANIA TUZO ZA EJAT

488c2eecfc8c3fb3aadb66e06249733b WAANDISHI 8 TSN WATEULIWA KUWANIA TUZO ZA EJAT

Thu, 17 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Waandishi wa Habari wanane wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) wameteuliwa kuwania Tuzo za Umahiri wa Habari nchini ( EJAT 2019 ) zitakazofanyika Septemba 28, mwaka huu jijini Tanga.

Waandishi hao ni Alfred Lastek, Baraka Messa, Evance Ng’ingo, Lucas Raphael, Sifa Lubasi na Kareny Masasi ( wote wa gazeti la Habarileo) wengine ni Sauli Gilliard na James Kamala wa gazeti la Dailynews.

Kamati ya Maandalizi ya tuzo hiyo ilitaja majina ya waandishi hao sambamba na waandishi wengine 48 kutoka vyombo vya habari mbalimbali nchini walioteuliwa kuwania tuzo hizo ambazo zimegawanywa kwa makundi 21.

Aidha Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye tuzo hizo.

Chanzo: habarileo.co.tz