Dunia imeshuhudia kupanda chati kwa J-pop (Japan), na K-pop (Korea Kusini), lakini je I-pop inaweza kuiteka dunia kwenye chati za muziki?
Hayo ndio matamanio ya kundi la wasanii wa kike lijulikanalo kama W.i.S.H ambayo ni kifupi cha World Inka Stage Hai, au maana yake kwa Kiswahili - “Dunia ni Jukwaa lao”.
Wanne hao waitwao – Ri, Zo, Sim na Suchi- wanasemekana kuwa kundi la kwanza kuu na wasichana kwa zaidi ya miaka 20.
India imekuwa na historia ya waimbaji wanawake, wakiwemo waimbaji kama Lata Mangeshkar, Asha Bhosle na Shreya Ghoshal.
Pia kuna akina dada wawili waliofanikiwa waitwao Nooran Sisters, lakini makundi ya wanawake hayajaweza kupenya vyema.
Zo ameiambia BBC Idhaa ya Asia kuwa W.i.S.H wanataka kubadilisha hali hiyo na kwenda hadi kileleni kwa kusambaza ujumbe chanya na uwezeshaji kwa wanawake.
Anaelezea kuwa ‘singo’ yao ya kwanza iitwayo Lazeez, ikimaanisha “tamu” kwa lugha ya Ki- Urdu, ni wimbo ambao “unasherekea mwanamke wa kisasa na kuhamasisha kujipenda”.
“Ni wa kipekee kwangu, na kwetu sote,” anasema.
Msanii Dilijit Dosanjh ni moja ya mfano wa jinsi nyota wa India wanaweza kuivutia dunia kwa kazi zao akifanya ushirikiano na wasanii kama Ed Sheeran na Sia.
***Kundi hilo katika picha- kutoka kushoto: Ri (Riya Duggal), Sim (Simran Duggal), Zo (Zoe Siddarth) na Suchi (Suchita Shirke).